Renato Sanches amekamilisha usajili wake wa kwenda Bayern Munich akitokea Benfica kwa ada ya uhamisho €35 million, baada ya kufukuziwa kwa muda mrefu na Manchester United.
Hivi hapa ni vitu 6 ambavyo unapaswa kufahamu kuhusu kiungo huyu mpya wa FC Bayern.
1)Alizaliwa mwaka 1997, atakuwa na miaka 19 ifikapo mwezi August.
2) Alijiunga na Benfica akiwa na umri wa miaka 9 mnamo mwaka 2006.
3) Mchezo wake wa kwanza wa kikosi cha kwanza cha Benfica ulikuwa mnamo October 30, 2015 akitokea benchi kwenye mchezo dhidi ya Tondela.
4) Ameshaichezea Ureno kupitia kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 19 na akaanza kukitumikia kikosi cha wakubwa mnamo March kwenye mchezo dhidi ya Bulgaria.
5) Vitor Paneira, kiungo wa zamani wa Benfica, amemuelezea mchezaji kwamba ni mchezaji wa matukio yote. Ujana wake unaleta utofauti kwenye timu. Ana uwezo wa kimwili na kiakili akiwavuruga timu pinzani katikati mwa uwanja.
No comments:
Post a Comment