Mbunge
wa Viti Maalum, Mariam Msabaha (Chadema) ametoa tuhuma nzito kuwa ndani
ya Bunge kuna wabunge vijana wanaovuta bangi na kutumia dawa za
kulevya.
Mbunge
huyo amemuomba Rais John Magufuli kuagiza wabunge wa aina hiyo ambao
hata hivyo hakuwataja wapelekwe Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili
kufundishwa nidhamu.
Msabaha
ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya
bajeti ya wizara ya Ulinzi na JKT iliyowasilishwa na Waziri mwenye
dhamana na Wizara hiyo, Dk Hussein Mwinyi.
“Wabunge
nao waende JKT kwa sababu hili Bunge wameingia vijana wengine ambao ni
mateja wa unga na wengine wanavuta bangi. Wengine wanawavua mama zao
nguo,” amesema Msabaha.
“Wengine
mama zao wameshakufa wanakuja humu wanawatukana mpaka wazazi wao. Kwa
hiyo niombe Rais Magufuli vijana wote wabunge ambao hawana nidhamu
waende JKT,” alisisitiza.
Mbunge
huyo amesema wabunge wa aina hiyo hawana viwango vya kuzungumza ndani
ya chombo hicho cha kutunga sheria hivyo ni vyema waende JKT ili
wakirudi wawe wamejua namna ya kuchangia.
Ingawa
hakumtaja Mbunge yeyote, lakini mchango ulioibua mtafaruku bungeni ni
wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyedai wabunge wa viti maalumu
Chadema huitwa Baby ili kupewa nafasi hiyo.
Tafsiri
ya kauli hiyo ni kuwa wabunge wa viti maalum Chadema lazima wafanye
mapenzi au kuwa na mahusiano na viongozi wa juu wenye mamlaka ndani ya
chama hicho ndipo wateuliwe kuwa wabunge.
No comments:
Post a Comment