Basi la Manchester
United lilishambuliwa kwa mawe lilipokuwa linaelekea katika uwanja wa
Upton Park ambao unamilikiwa na wapinzani wao katika mechi ya jumanne
jioni West Ham.
Shambulizi hilo lilisababisha mechi baina ya Manchester United na West ham kucheleweshwa kwa zaidi ya dakika 45.Mechi ilikuwa imeratibiwa kuanza saa tatu na dakika 45 lakini ikaanza saa nne u nusu.
Basi hilo lilishambuliwa kwa chupa na mawe.
Madirisha yake yalivunjika baada ya shambulizi hilo lililolazimu askari wa kupambana na ghasia kuwalinda na kuwasindikiza Manchester united hadi Uwanjani Upton Park.
''ilikuwa tukio la kushtua sana , haikufurahisha kabisa kushambuliwa na mashabiki wa timu pinzani hadi gari letu linaharibiwa'' alisema nahodha wa Manchester United Wayne Rooney
Ninaamini West Ham hawatafurahia kuona walichofanya mashabiki wao.
Hii ndio mechi ya mwisho kwa West ham kutumia uwanja huo wa Upton kwa mechi zao za nyumbani.
Timu hiyo inatarajiwa kuhamia makao yao mapya ya Olympic Stadium.
West Ham imekuwa Upton Park, kwa miaka 112 .
Aidha uwanja huo wa Upton unafahamika pia kama Boleyn Ground.
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal alinukuliwa akisema kuwa hana cha kusema ila angependa picha zenyewe zijieleze.
''Bila shaka itaathiri matokeo yetu uwanjani,mashabiki hawa walijawa na hasira sana'' alisema Van Gaal
No comments:
Post a Comment