Tuesday, 10 May 2016

Mama afichua pacha wake watano Australia

Mama mmoja raia wa Australia ametoa picha za mapacha watano aliowazaa mwezi Januari.Kim Tucci wa miaka 26 alichukua dadika mbili tu kujifungua wanawe hao, wasichana wanne na mvulana mmoja.
Wote walitungwa kawaida, hakutumia matibabu yeyote ya uzazi.
Madaktari 50 walimsaidia mama huyo kujifungua kwa njiya ya upasuaji, na wanawe wote wako shwari.Wanasayansi wanasema ni mama mmoja kati ya milioni 55 ana nafasi ya kuzaa mapacha watano.
Bi Tucci alipata umaarufu sana wakati alipoweka taarifa za mimba yake katika ukurasa wake wa Facebook.Kampuni ya kunasa picha ya Erin Elizabeth imesaidia sana kunadi safari ya Bi Tucci wakati wa uja uzito wake.
Mama huyo ameelezea changamoto alizokumbana nazo akisema kwa wakati mmoja alihisi kama anapoteza maisha.Ameongeza madaktari walimshauri kuwaokoa watoto wawili na kumtaka kuwatoa wengine kutokana na sababu za kiafya.
Hata hivyo aliamua kubeba mimba yake hadi mwisho.
Bi Tucci na mumewe bwana Vaughn wana watoto watatu mvulana na wasichana wawili.Wameanza kuchangisha pesa ili kununua gari kubwa ambalo litaweza kukimu familia hiyo kubwa.

No comments:

Post a Comment