Klabu ya ndio mabingwa wa ligi kuu ya uingereza ‘English Premier league’ 2015/2016/.
Klabu hiyo ilikabidhiwa kombe lao la kwanza la ligi hiyo siku ya jana baada ya mechi dhidi ya Everton ambapo pia waliibuka na ushindi wa 3 – 1.
Leicester City ilitwaa taji hilo moja kwa moja baada ya Tottenham Hotspurs kutoka sare ya 2-2 na Chelsea wiki iliyopita.
Kombe la kwanza la Ligi Kuu kwa klabu ya Leicester City iliyoanzishwa miaka 132 iliyopita, lakini pia hili ndio taji la kwanza la Ligi Kuu kwa kocha wao Claudio Ranieri ambaye amewahi kuvifundisha vilabu ya Napoli, Inter Milan, Chelsea, Atletico Madrid na Juventus.
Leicester City haikuwahi kushinda ubingwa wa ligi kuu Uingereza tangu klabu hiyo iliyoanzishwa miaka 132 iliyopita.
No comments:
Post a Comment