Bunge la 11 limeendelea tena Dodoma leo Mei 5 2016, Katika Kipindi cha Maswali ya papo kwa pako kwa Waziri Mkuu Mbunge Sikonge Joseph kakunda amemuuliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa..>>>
‘Kumekuwa
na migogoro ya Wakulima na wafugaji kugombea maeneo nchini, katika
ilani ya uchaguzi kuna maelekezo kwamba Serikali itapima maeneo mapya,
Je, ni lini Serikali hii kazi itatekelezeka?’
Waziri Majaliwa akijibu kwa kusema.. >>’Nikiri
kwamba sasahivi tuna migogoro mingi sana ya wafugaji na wakulima lakini
pia migogoro ya jamii na jamii, Jambo ambalo amelieleza Mbunge ni
miongoni ya mikakati tuliyonayo pia’
‘Tumeanza
kutafuta njia sahihi ya kuondoa migogoro ya ardhi, lakini wakati
mwingine ni kutokana na utendaji wa hovyo wa watendaji wetu wa Serikali
tuliowapa dhamana’
‘Tunao
wawekezaji wanaoingia kinyemela kwenye maeneo yetu na kujichukulia
maeneo na kusababisha migogoro, Kwanza tumezipa maagizo Wizara zote
husika watupe maeneo ya mipaka’
No comments:
Post a Comment