Tuesday, 18 October 2016

Diamond na Harmonize washinda tuzo Marekani

Harmonize (kushoto) na Tekno kutoka Nigeria


Afrika Mashariki imekuwa na furaha kubwa wikendi kwenye tuzo za kila mwaka za Jarida la mziki Afrika, maarufu kama Afrimma Awards baada ya wasanii wa Kenya na Tanzania kuzoa tuzo tofauti kwenye hafla iliyofanyika Marekani wikendi.
Imekuwa ni ushindi mkubwa kwa Wasanii wa lebo ya Wasafi kutoka Tanzania, Diamond Platnumz na Harmonize walioibuka mabingwa kwenye vitengo vyao.
Diamond alimshinda Mtanzania mwenzake, Ali Kiba katika kitengo cha mwanamuziki bora wa kiume Afrika Mashariki.
Harmonize, anayezidi kuvuma kwa wimbo wake wa 'Inde' aliomujmuisha Dully Sykes, akitunukiwa tuzo ya Msanii mpya wa mwaka.
Hata hivyo Diamond hakuweza kuhifadhi taji lake la msanii bora wa mwaka aliloshinda mwaka wa 2015 kwani tuzo hiyo ilikwenda kwa Mnigeria Falvour.
Kwa upande mwingine, Kenya ilipata tuzo tatu kupitia Msanii wa nyimbo za injili, Willy Paul, aliyeshinda kitengo cha msanii bora wa injili nalo kundi la Sauti Soul likapewa tuzo ya kundi bora la mwaka.

Mwanamuziki wa kike, Akothee, aliondoka na taji la mwimbaji bora wa kike licha ya mashabiki kutishia kutompigia kura

No comments:

Post a Comment