Tuesday, 18 October 2016
JUMATANO NOU CAMP: BARCA KUIVAA CITY YA GUARDIOLA!
MOJA ya Mechi za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, za Wiki hii zenye mvuto mkubwa ni ile ya Jumatano huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain kati ya FC Barcelona na Manchester City ikiwa ni Mechi ya Kundi C.
Mvuto mkubwa ni Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola, kuiongoza Timu yakekutua Nou Camp mahala ambapo ndio chimbuko lake.
Akiwa na Barca kama Mchezaji, Guardiola alitwaa Ubingwa wa La Liga mara 6 na wa Ulaya mara 1 na alipokuwa Kocha Mkuu wa Timu hiyo alizoa Makombe 14 yakiwemo Mawili ya UCL.
Mara ya mwisho kwa Guardiola kuiongoza Timu nyingine kucheza na Barca huko Nou Camp ilikuwa Msimu wa 2014/15 alipokuwa na Bayern Munich na kuchapwa 3-0 kwenye Nusu Fainali ya UCL.
Kwenye Kundi C la UCL, Barcelona ndio Vinara baada ya kushinda Mechi zao zote 2 za kwanza na Man City wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma baada ya kutoka Sare 3-3 na Celtic kwenye Mechi yao iliyopita.
+++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Barcelona imeifunga Man City Mechi zao zote 4 zilizopita za Mashindano rasmi.
+++++++++++++++++++
Wikiendi hii iliyopita, Man City walitoka Sare 1-1 na Everton kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, ambayo Wachezaji wao Kevin De Bruyne na Sergio Aguero walikosa Penati zilizookolewa na Kipa na pia hiyo kuwa Mechi yao ya 3 mfululizo kutoka Sare.
Wikiendi, Barcelona waliinyuka 4-0 Deportivo La Coruna huku Rafinha akipiga Bao 2 na Staa wao mkubwa, Lionel Messi, alieanzia Benchi baada ya kuwa nje alipoumia Nyonga, alifunga Bao 1.
Kwenye Mechi na Everton, Guardiola alitumia Mfumo wa 3-4-3 lakini huko Nou Camp ataanza na Mabeki Wanne huku Pablo Zabaleta akianza kama Fulbeki wa Kulia kuchukua nafasi ya Bacary Sagna ambae pia aliikosa Mechi na Everton kutokana na maumivu.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
BARCELONA: Bravo, Mathieu, Mascherano, Pique, Digne, Iniesta, Busquets, Rakitic, Messi, Suarez, Neymar
MAN CITY: Bravo, Zabaleta, Otamendi, Kompany, Clichy, Fernandinho, Gundogan, Sterling, Silva, De Bruyne, Aguero
REFA: Milorad Mažić (Serbia)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Ratiba:
Jumanne Oktoba 18
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI E
Bayer Leverkusen v Tottenham
CSKA v Monaco
KUNDI F
Real Madrid v Legia Warsaw
Sporting Lisbon v Borussia Dortmund
KUNDI G
Club Brugge v FC Porto
Leicester v FC Copenhagen
KUNDI H
Dinamo Zagreb v Sevilla
Lyon v Juventus
Jumatano Oktoba 19
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI A
Arsenal v Ludo Razgrad
Paris St Germain v Basel
KUNDI B
Dynamo Kiev v Benfica
Napoli v Besiktas
KUNDI C
Barcelona v Man City
Celtic v Borussia Monchengladbach
KUNDI D
Bayern Munich v PSV Eindhoven
FC Rostov v Atletico Madrid
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:
Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba
Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba
Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba
Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba
Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba
Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba
MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment