Magoli ya Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo yametosha kuifanya
Simba iendeleze ubabe mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kuifunga kwa mara
nyingine tena kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Magoli yote ya Simba yamefungwa katika kipindi cha pili baada ya timu hizo kutoka suluhu katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Mchezo huo uliwafanya Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya
kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar tangu wajiunge na Simba
msimu huu wa dirisha la usajili.
Mohamed Ibrahim ni mchezaji mwingine ambaye alisajiliwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa lakini hakupata nafasi ya kucheza.
Dondoo kwa namba
30 Namba kubwa zaidi ya jezi ilivaliwa na golikipa wa Mtibwa Sugar Abdallah Makangana.
10 Pointi ambazo Simba imefikisha baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa.
6 Pointi za Mtibwa baada ya kucheza mechi nne. Imeshinda mechi mbili na kupoteza michezo miwili.
9 Mtibwa wapo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi baada ya mchezo dhidi ya Simba.
2 Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 10 sawa na Azam FC wanaoongoza ligi.
Katika mechi saba zilizopita, Mtibwa haijapata ushindi
ushindi dhidi ya Simba. Imetoka sare kwenye mechi mbili na kupoteza
mechi tano.
Rekodi za Simba vs Mtibwa Sugar
11/09/16 Simba 2-0 Mtibwa Sugar
15/05/16 Mtibwa Sugar 0-1 Simba
16/01/16 Simba 1-0 Mtibwa Sugar
14/03/15 Simba 1-0 Mtibwa Sugar
01/11/14 Mtibwa 1-1 Simba
05/02/14 Mtibwa Sugar 1-1 Simba
14/09/13 Simba 2-0 Mtibwa Sugar
No comments:
Post a Comment