Wednesday, 7 September 2016

Syria kumaliza mapigano

Syria
Askari upande wa upinzani akijihami
Makundi ya upinzani nchini Syria yametoa mapendekezo ya kina juu ya kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa zaidi ya kipindi cha miaka mitano.
Katika kikao cha maridhiano kilichofanyika jijini London, wakisaidiwa na kamati kuu ya maridhiano ya Saud rais Bashar al-Assad amesema, mazungumzo yataendelea baada ya miezi 6 ya kwanza ya mpito.Mapema serikali ya Syria ilieleza kuwa madai ya kuondolewa kiongozi wa nchi aliyechaguliwa ni ya kijinga.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa upinzani unafahamu rais Assad hawezi kuhiari kukaa kando. Lakini wanatumaini kuwa kipindi cha mpito kitasaidia kuzishawishi pande zinazo hasimiana za Urusi na Iran, kuweka shinikizo kwa kiongozi wa Syria.BBC

No comments:

Post a Comment