Wednesday, 7 September 2016

SIMBA 2-1 RUVU SHOOTING FULL TIME 'LIVE' KUTOKA UWANJA WA UHURU

Image result for simba klabu 2016 / 2017

Dakika 90 + 2: Mwamuzi anamaliza mchezo. Simba inapata ushindi wa mabao 2-1.


Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.

Dakika ya 88: Matokeo bado 2-1, Simba inaongoza na mchezo unaendelea.

Dakika ya 85: Issa Kanduru wa Ruvu anamchezea faulo Mohammed Hussein, anapewa kadi ya njano.

Dakika ya 85: Mchezo umetawaliwa na faulo za hapa na pale.
 
Dakika ya 84: Beki wa kati wa Simba, Lufunga anacheza faulo katikati ya uwanja, anapewa kadi ya njano.

Dakika ya 82: Simba wanafanya mabadiliko, Kichuya anatoka, anaingia Jamal Mnyate.

Dakika ya 79: Kiungo wa Ruvu, Jabir Azizi anamchezea faulo Mzamiru, anapewa kadi ya pili ya njano kisha mwamuzi anampa kadi nyekundu na kumtoa nje.

Dakika ya 73: Blagnon anapewa kadi ya njano kwa kusukuma kipa wa Ruvu.

Dakika ya 73: Blagnon na Ajib wanapata nafasi ya wazi lakini wanakosa, baada ya mpira uliopiga na Ajibu kugonga mwamba kisha kipa wa Ruvu akaokoa. 

Dakika ya 71: Said Ndemla anatoka anaingia Mzamiru Yasin.

Dakika ya 69: Ndemla anapewa kadi ya njano kutokana na kuonyesha mchezo mbaya.


Dakika ya 67: Mavugo anaenda kupumzika katika benchi na nafasi yake inachukuliwa na Blagnon.

Dakika ya 60: Ruvu wanapambana kutafuta bao la kusawazisha lakini viungo wakabaji na mabeki wa Simba wanaonyesha kuwa imara.

Dakika ya 51: Ruvu wanamtoa Abrahman Mussa anaingia Baraka Mtuwi.

Mashabiki wa Simba wananyanyuka na kushangilia baada ya kupata bao hilo la pili. Shangwe zimeongezeka sasa!

Dakika ya 48: Mavugo anaipatia Simba bao la pili baada ya kumalizia mpira mzuri aliopigiwa na Ajib.



Kipindi cha pili kimeanza.

Kipindi cha kwanza kimekamilika, matokeo ni bao 1-1. Timu zimeingia kwenye vyumba kupumzika.

Dakika 45: Bado timu zote zinasomana na kushambuliana kwa zamu.

Dakika ya 43: Mavugo anatupia mpira wavuni lakini anakuwa ameshaotea. Mwamuzi wa pembeni anasimama kuonyesha Mavugo aliotea kabla ya kuupiga mpira.
 
Dakika ya 35: Timu zote zinashambuliana kwa zamu, Simba wanatengeneza nafasi kadhaa lakini wanashindwa kuzitumia vizuri.

Dakika ya 29: Ruvu wanafanya mabadiliko, wanamtoa Frank Msese anaingia Renatus Kisase.

Dakika ya 26: Claide Wigenge wa Ruvu anapiga shuti kali lakini kipa wa Simba, Angban anaokoa.
 
Dakika ya 24: Ajib anafanya kazi nzuri, anaingia na mpira, anampasia Lavugo ambaye anashindwa kutumia vizuri nafasi hiyo.
 
Dakika ya 20:Mavugo anakosa nafasi ya wazi akiwa ndani ya eneo la 18, shuti lake linatoka nje kidogo ya lango.

Dakika ya 18: Mchezo umechangamka na timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 15: Mchezo unaendelea na una kasi kubwa.
Dakika ya 11: Ibrahim Ajib anaisawazishia Simba baada ya kufunga bao zuri akiunganisha krosi ya Mohamed Hussein.
Dakika ya 10: Simba wanafanya mashambulizi kadhaa katika kutaka kusawazisha lakini Ruvu wanakuwa wagumu.
Dakika ya 8: Abraham Mussa anaifungua Ruvu bao la kwanza baada ya mabeki wa Simba kufanya uzembe wa kumkaba. Ruvu wanaongoza bao 1-0.
Mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba na Ruvu Shootingi unatarajiwa kuchezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru hapa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Simba kilichoanza leo:
Angban, Malika Ndeule, Mohamed Hussein, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Kichuya, Said Ndemla, Ladius Mavugo, Ibrahim Ajib na Mwinyi Kazimoto.


Kikosi cha Ruvu:
Rashid, Makwaya, Msese, Bofu, Nayopa, Jabir, Mussa, Kisiga, Dilunga, Maganga, Wigenge.

No comments:

Post a Comment