Wednesday, 7 September 2016

DONDOO MUHIMU KUELEKEA MANCHESTER DERBY

Manchester derby

Kwenye El Classico Barcelona ya Pep Guardiola ilikua na rekodi nzuri dhidi ya Madrid ya Jose Mourinho. Sasa makocha hawa wapo nchini Uingereza, Guardiola akifundisha Manchester City wakati Mourinho akiwa Manchester United.

Baada ya kila mmoja kushinda mechi tatu za mwanzoni ligi kuu England 2016/17 timu zao zinakutana kwenye mechi ya nne  siku ya Jumamosi ndani ya dimba la Old Trafford. Kuelekea mechi hii makala hii inakupa baadhi ya dondoo katika mtindo wa namba.
Namba 16
Ni idadi ya mechi ambazo zimewakutanisha makocha Pep Guardiola dhidi ya Jose Mourinho. Pep Guardiola amefanikiwa kushinda mechi saba (7) huku Jose Mourinho akishinda mechi tatu (3), Mechi sita  (6) zilimalizika kwa sare.
Jose Mourinho amekutana na Pep Guardiola akiwa na timu za Real Mardid na InterMilan.  Mara zote ambazo wamekutana Pep Guardiola alikuwa na klabu ya Barcelona
Namba 38
Idadi ya mechi ambazo Man Utd wamekutana na City kwenye ligi kuu England tangu msimu wa mwaka 1992/93. Man United imeshinda mechi ishirini (20) wakati City imeshinda mechi kumi na moja (11) huku mechi saba (7)  zikimalizika kwa sare
Namba 9
Ni mabao ya kufunga ya timu ya Man City ndani ya mechi tatu. Hakuna timu yoyote ambayo imefikisha idadi hiyo ya mabao hadi sasa. Pia Man City imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara tatu (3)
Namba 2
Mechi ambazo Man United wamecheza bila kuruhusu wavu wao kutikisika. Walifanya hivyo kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton pamoja na mechi ya Hull City ambao Utd ilishinda 1-0
Pia kiungo wa City Kevin De Bruyne pamoja wa washambuliaji wa Man Utd Rooney na Antony Martial wametoa pasi mbili za mabao kila moja.
Namba 50
Hadi sasa mshambuliaji wa Man Utd  Zlatan Ibrahimovic amechangia asilimia  hamsini (50%)  ya mabao ya kufunga ya timu yake. Ibrahimovic amefunga mabao matatu (3) sawa na mshambuliaji wa Man City Aguero ambaye atakosekana baada ya kupewa adhabu ya mechi tatu na chama cha soka nchini England FA.
Namba 15
Mshambuliaji Sergio Aguero wa Man City ndiye aliyepiga mashuti mengi hadi sasa kwenye ligi kuu nchini England. Aguero amepiga mashuti 15 wakati mshambuliaji wa Man United Zlatan Ibrahimovic amepiga mashuti 12
Namba 2
Mwamuzi Mark Clattenburg ambaye atachezesha mechi ya Jumamosi kwa siku za karibuni amechezesha mechi mbili za Manchester Derby. Mechi ya kwanza msimu wa 2014/15 Man Utd ilishinda 4-2. Pia mwezi October 2015 alichezesha Derby ambayo iliisha kwa sare ya 0-0.
Namba 1
Man City inashika nafasi ya kwanza kwenye ligi ikiwa na alama tisa (9) baada ya mechi tatu (3). Man Utd inashika nafasi ya tatu (3) ikiwa na alama tisa(9). Man City wapo kileleni kwa wiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Namba 1761
Man City ndiyo timu inayoongoza kwa kupiga pasi nyingi hadi sasa. Ndani ya michezo mitatu wamepiga idadi ya pasi 1761. Nafasi ya pili inashikiliwa na Liverpool ikifuatiwa na Chelsea pamoja na Southampton. Man United inashika nafasi ya tano ikiwa na jumla ya pasi 1584
Namba 11
Mshambuliaji wa Man United Wyne Rooney ndiye anashilikia rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye pambano la Manchester Derby. Hadi sasa amefunga mabao 11.

No comments:

Post a Comment