Wednesday, 7 September 2016

YANGA YASHINDWA KUTOBOA REKODI MTWARA

IMG_0016

Uwanja wa Nangwanda Sijaona umeendelea kuwa mgumu kwa Yanga baada ya kushindwa kupata ushindi kwa mara nyingine kufuatia kulazimishwa suluhu na Ndanda kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania.

Mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda, Yanga walichezea kipigo cha goli 1-0 ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Ndanda kucheza dhidi ya Yanga ntangu walivyopanda daraja.

Mshambuliaji wa Yanga Obrey amecheza kwa mara ya kwanza mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wakati Yanga ikicheza dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara
Mshambuliaji wa Yanga Obrey amecheza kwa mara ya kwanza mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wakati Yanga ikicheza dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara
Golikipa wa Ndanda FC Jeremia Kisubi alikuwa akipoteza muda kwenye mchezo dhidi ya Yanga na kupelekea mwamuzi kutoa adhabu ya mkwaju wa adhabu ndogo ndani ya eneo la 18 baada ya kipa huyo kudaka mpira na kukaa nao kwa muda

Matokeo hayo yameendelea kuzifanya timu hizo huongeza idadi ya michezo waliyotoka sare. Ndanda na Yanga zimeshakutana mara 5 hadi sasa, Yanga imeshinda mechi moja sawa na Ndanda ambayo nayo imeshinda mechi moja huku timu hizo zikiwa zimetoka sare michezo mitatu.

Donald Ngoma (kushoto) akiwania mpira na beki wa Ndanda FC
Donald Ngoma (kushoto) akiwania mpira na beki wa Ndanda FC
Ndanda ikiwa inacheza mchezo wake wa kwanza kwenye uwanja wa nyumbani iliweza kuhimili mashambulizi ya Yanga ambayo pia ilikuwa ikicheza mchezo wake wa kwanza ugenini tangu kuanza kwa ligi msimu wa 2016-2017.
Licha ya kufanya mashambulizi ya mara kwa mara, wachezaji wa Yanga walishindwa kupata goli na kujikuta wakipata kona nyingi kutokana na walinzi wa Ndanda kuokoa mashambulizi ya hatari yaliyofanywa na Yanga.

SalumTelela amecheza mechi yake ya kwanza dhidi ya imu yake ya zamani (Yanga) ikiwa ni baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu sita mfululizo
SalumTelela amecheza mechi yake ya kwanza dhidi ya imu yake ya zamani (Yanga) ikiwa ni baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu sita mfululizo

No comments:

Post a Comment