Sunday, 14 August 2016
SIMBA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA WATOZA KODI WA UGAND
Wekundu wa Msimbazi Simba leo wamelazimishwa sare goli 1-1 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.
URA walianza kupata bao lililofungwa na Nkugwa Elkanah 19kipindi cha kwanza lakini Jonas Mkude alisawazisha bao hilo dakika ya 31 kwa kuunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na beki wa kushoto Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr.
Mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa ni ya pili kwa Simba baada ya klabu hiyo kucheza mchezo mwingine August 8 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya wakati wa maadhimisho ya Simba Day.
Katika mcchezo dhidi ya Leopards ya Kenya, Simba ilipata ushindi wa magoli 4-0 yaliyofungwa na Ibrahim Ajib ambaye alifunga mawili, Shiza Kichuya na Laudit Mavugo lakini leo nyota hao hawakufanikiwa kufunga bao.
Simba inajiandaa na ligi kuu ya soka Tanzania bara inayotarajiwa kuanza Agust 20, Simba itaanzia kwenye uwanja wa taifa dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment