MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amesema Paul Pogba yuko tayari kucheza Mechi na Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’, Ijumaa Usiku ingawa anaweza asionyeshe cheche zake.
Pogba, mwenye Miaka 23 na ambae sasa ndie Mchezaji wa Bei Ghali Duniani kufuatia Dau la ununuzi wake kutoka Juventus, aliikosa Mechi ya kwanza ya Man United Wikiendi iliyokwisha akiwa Kifungoni Mechi 1 kutokana na Kadi za Njano 2 alizopata huko Italy Msimu uliopita.
Kufuatia Uhamisho wake kuchelewa kukamilika kutokana na kuwa Vakesheni iliyopitiliza kutokana na ushiriki wake kwenye EURO 2016 akiichezea Nchi yake France, Pogba amekuwa Mazoezini na Man United kwa Siku 11 tu.
Lakini Mourinho anaamini Pogba yuko tayari kucheza Mechi hiyo ya Ligi Kuu England, EPL, dhidi ya Southampton hata kama hatadumu Dakika 90.
Mourinho ameeleza: “Tulipocheza na Leicester walikuwepo Wachezaji ambao walikuwa na Mazoezi kidogo kupita Pogba.”
Akiongea na Wanahabari hii Leo kuhusu Mechi yao ya Ijumaa, Mourinho alieleza Pogba amefanya Mazoezi kwa Siku 11 na imekuwa rahisi kumbadili Pogba kwa vile ni Kijana aliekulia Old Trafford na anamjua kila Mtu.
++++++++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Southampton wamekuwa wakizoa Pointi 3 Old Trafford kila mara kwa Misimu Miwili sasa wakiungana na Norwich, WBA na Swansea kwa hilo.
++++++++++++++++++++++++++++++
Alipoulizwa kama yeye anaweza kusaidia kurejesha ile hali ya Timu kuiogoga Man United iliyokuwepo enzi za Sir Alex Fergosn, Mourinho alijibu: “Sio mimi. Ni Timu, ndio. Na Mashabiki pia. Nadhani kila kitu kinaanza hapo, uhusiano kati ya Timu na Mashabiki.”
Aliongeza: “Ikiwa humo Old Trafford, Mashabiki wa Upinzani, Maelfu kadhaa wanakuwa na kelele kubwa kupita Mashabiki zaidi ya Elfu 70, basi sisi tupo mashakani. Inamaanisha uhusiano kati ya Timu na Mashabiki wake. Kukiwepo uhusiano, basi ule ukweli wa kutisha tukiwa Nyumbani utarudi. Kila kitu kinaanza na uhusiano huo wa Timu na Mashabiki wake. Ikiwa Mashabiki watahusiana na Timu, wanataka nao kucheza, na wakicheza, Wapinzani hawana nafasi!”
LIGI KUU ENGLAND
Msimu Mpya 2016/17Ratiba:
**Saa za Bongo
Ijumaa Agosti 19
2200 Man United v Southampton
Jumamosi Agosti 20
1430 Stoke City v Man City
1700 Burnley v Liverpool
1700 Swansea v Hull
1700 Tottenham v Crystal Palace
1700 Watford v Chelsea
1700 West Brom v Everton
1930 Leicester City v Arsenal
Jumapili Agosti 21
1530 Sunderland v Middlesbrough
1800 West Ham v Bournemouth
No comments:
Post a Comment