Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha site Mirror zilizoibwa katika magari leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya Operesheni mbalimbali za kanda hiyo pamoja na kuzuia maandamano ya UKUTA, jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha magazine ya kuwekea risasi zilizokamatwa jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akioyesha bastola aina ya Browning yenye risasi sita iliyokamatwa jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha flana rangi mbalimbali zilizokamatwa.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya
Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) yanayopangwa kufanyika
Septemba 1 mwaka huu. Maandamano hayo yamepewa jina la UKUTA ambapo
wanachama wake wanataka kuingia mitaani kupinga kile wanachokiita
ukandamizaji wa demokrasia.
Kamanda
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema leo kwamba
maandamano hayo hayatafanyika na jeshi la polisi limejipanga kuzuia
maandamano hayo.
Kamanda
Sirro amesema kuwa hakuna habari ya Ukuta na hakuna mtu atakayedhubutu
kuingia barabarani kutokana jeshi lilivyojipanga kuhakikisha wananchi
wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa na kitu chochote.
Amesema kuwa utaratibu wa kufanya mikutano ya siasa umeelezwa hivyo kufanya mikutano bila kufuata utaratibu hautaruhusiwa.
Kamishina
Sirro amesema kuwa kikundi/watu wanaotaka kutumia siasa katika kuvunja
Amani kwa Dar es Salaam hakuna kitu chochote kitafanyika kutokana na
jeshi la polisi lilivyojipanga.
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Agasti 20 majira ya saa 12:00 jioni
lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya mtaa wa Ufipa
Kinondoni kuna duka linauza flana rangi mbalimbali zenye maneno ya
uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ rangi
nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye maneno ‘UKUTA’
fulana 6 za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi nyeusi
23 zenye maneno ’’UKUTA’’.
Aidha
Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata
mtuhumiwa Yoram Sethy Mbyelllah (42) mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati
akiwa anauza fulana hizo dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na
baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment