Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa wodi katika zahanati ya Inyonga
wilayani Mlele amabayo inatarajiwa kupandishwa hadhi na kuwa hospitali
ya wilaya . Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti22, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa Inyonga
baada ya waziri Mkuu kutawazwa kuwa Chief wa Wakonongo na kupewa jina la
Chief Kayamba wa Kwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
uwanja wa Shule ya Msingi Inyonga Agosti 22, 2016. Kulia ni Cheif wa
Wakonongo, Kayamba wa Pili.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
ambaye pia ni Mbunge wa Katavi, Mhandisi Isaack Kamwelwe katika mkutano
wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Inyonga
wilayani Mlelele Agosti 22, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Inyonga wilayani Mlele Agosti 22, 2016.
No comments:
Post a Comment