Wednesday, 31 August 2016

LEO MWISHO UHAMISHO: NASRI, CHAMBERS WAKOPESHWA, LUIZ KURUDI STAMFORD BRIDGE?

DAVID-LUIZ

LEO ndio Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho ambalo litafungwa rasmi Saa 7 Usiku Saa za Bongo na zipo dili kadhaa zimekamilika na nyingine zikisukwa za Dakika za mwisho na nyingine zinatarajiwa kuwa za kushtukiza.
PATA BAADHI YA HIZO:
BORO YAMSAINI KWA MKOPO CHAMBERS WA ARSENAL
Middlesbrough wamemsaini Beki wa Arsenal Calum Chambers kwa Mkopo wa Msimu mmoja.
Chambers, mwenye Miaka 21 na ambae ana uwezo wa kucheza kama Fulbeki wa Kulia au Sentahafu, alijiunga na Arsenal Mwaka 2014 kutoka Southampton kwa Dau la Pauni Milioni 16.
Chambers anakuwa Mchezaji wa 11 kusainiwa na Meneja wa Boro Aitor Karanka wakiwemo Kipa Victor Valdes, Straika Alvaro Negredo na Kiungo Marten de Roon.
LUIZ KURUDI CHELSEA
David Luiz huenda akarejea Chelsea baada kuibuka ripoti kuwa Klabu hiyo iko tayari kuilipa Paris Saint-Germain Pauni Milioni 30.
Luiz, Raia wa Brazil mwenye Miaka 29, aliuzwa na Chelsea huko PSG Miaka Miwili iliyopita kwa Dau la Pauni Milioni 50 ambalo lilikuwa ni rekodi kwa Beki kunuliwa Bei ghali kiasi hicho.
Inaaminika Meneja Mpya wa Chelsea Antonio Conte anasaka Sentahafu baada ya kuwakosa walengwa wake Alessio Romagnoli wa AC Milan na Kalidou Koulibaly wa Napoli.
Chelsea walimnunua Luiz kwa mara ya kwanza Januari 2011 kutoka Benfica kwa Pauni Milioni 21 na akadumu Miaka Mitatu na kucheza Mechi 143 akifunga Bao 12.
NASRI MKOPO SEVILLA
Manchester City wamekubali Samir Nasri aende Sevilla ya Spain kwa Mkopo.
Sevilla inatarajiwa kuwa itamlipa Nasri, mwenye Miaka 29, Asilimia 65 ya Mshahara wake na nyingine kulipwa na City.
Pep Guardiola alipitua City hivi karibuni Nasri alitupwa nje ya Kikosi cha Kwanza na kulazimika kufanya mazoezi peke take baada ya Meneja huyo kudai amekuwa mnene mno.
Lakini Jumamosi Nasri aliingizwa kutoka Benchi wakati City ikiichapa West Ham 3-1 huko Etihad.

No comments:

Post a Comment