Wednesday, 31 August 2016

CHELSEA WANASA KITASA CHA FIORENTINA

1
Chelsea wamethibitisha kumsajili beki Marcos Alonso kutoka Fiorentina ya Italy kwa ada ya paundi mil 23.
Alonso hatakuwa mgeni kwenye Ligi ya England baada ya hapo awali kuwahi kucheza katika vilabu vya Bolton na Sunderland.

Usajili huo hauishii hapo kwa Chelsea kwani bado wanahusishwa na mipango ya kumrejesha beki wao wa zamani David Luiz kwa ada ya paundi mil 32 ambaye miaka miwili iliyopita walimuuza kwenda PSG kwa ada ya paundi mil 50.
Wakati huo huo, winga wao Juan Cuadrado amerudi tena Juventus kwa mkopo wa msimu mzima.

No comments:

Post a Comment