Asilimia kubwa ya bishara nyingi zinazo anzishwa
hushindwa kuendelea zaidi ya mawaka mmoja hii inatokana na kushindwa
kuzingatia mambo ya msingi yanayoweza kuimarisha biashara yako.
Unapotaka kuanza biashara yoyote kuna mambo muhimu ya kufanya kabla
hujaanza ili kujenga msingi mzuri wa biashara yako na kuhakikisha kuwa
inasimama na kukua vizuri ili kukupatia kipato endelevu.
Leo tutaangalia hatua za muhimu kufuata unapotaka kuanzisha biashara yako.
- Buni wazo la biashara yako.
Kupata wazo zuri la biashara ni hatua ya kwanza na ya muhimu katika
kuanzisha biashara yako. Unatakiwa kuorodhesha biashara zilizopo kwenye
soko unalolikusudia kulifikia, hii itakusaidia kujua ni biashara gani
unaweza kuifanya na ipi hutaweza kuifanya na zaidi sana itakuonesha
biashara ambayo haijafanywa na inaweza kuwa na uhitaji katika eneo lako.
Unaweza kupata hata mawazo matatu ya biashara.
- Fanya utafiti wa masoko.
Kabla hujaamua ni biashara ipi uifanye unatakiwa kufanya utafiti kwa
watu wanofanya biashara kama hiyo unayotaka kuanzisha. Njia nzuri ni
kuuliza watu wanofanya biashara kwenye maeneo mengone tofati na
unapolenga kufanyia biashara. Hii itakusaidia kupata ujuzi wa masoko,
changamoto na fursa zilizopo katika biashara unayokusudia kufanya.
Sehemu nyingine ya kuweza kupata ushauri ni kwenye mitandao ya kijamii
na kwenye tovuti kama
Jamii forum.
- Andaa mpango wa biashra yako.
Jambo lingine la muhimukufanya ni kuandaa mpango wa biashara yako.
Mpango wa biashara ni mpangilio mzima wa biashara yako unaoelezea
unafanya biashara gani, wamiliki wa biashara, unahitaji nini ili uanze,
gharama za undeshaji wa biashara yako, makadirio ya mapato ya biashara
yako, kiasi cha mtaji mkinachi hitajika kuanza, vyanzo vya mtaji na
malengo ya biashara yako. Mpango wa biashara ni lazima uwe kwenye
maandishi ili uwe rahisi kuufutilia na kufanya marekesbisho
yanapohitajika.
- Sajili biashara yako.
Kitu cha muhimu kabla ya kuanzisha biashara yako ni kuhakisha kuwa
umekwisha kuisajili na kupata lesseni na vibali husika. Usajili wa
bishara hufanyika kwenye ofisi za msajili wa makampuni maarufu kama
BRELA. Namba za utambulisho wa mlipa kodi hupatikana katika ofisi ya TRA
iliyokaribu na wewe. Pia leseni na vibali hutolewa na halmashauri za
wilaya husika na wakati mwengine mamlaka kwa mfano biashara za chakula
ni lazima kupata viabali vya TFDA.
- Anza biashara yako.
Baada ya kuanda mpango wa biashara yako kinachofuata ni kukusanya
mtaji wako wa kuanzisha biashara yako, andaa sehemu ya kufanyia kazi,
tafuta vifaa vya kufania kazi, tafuta watu wa kukusaidia kama
watahitajika. Kitu cha muhimu ni kuanza biashara yako mapema iwapo unazo
rasilimali za kutosha kuanza, si lazima uwe na mtaji mkubwa sana ili
uanze, biashara yako inaweza kukua na kukupatia mtaji wa kufikia
malengo yako.
- Tangaza biashara
Waswahili husema biashara ni matangazo. Hii haina kificho kwa watu
wasipojua unachofanya kamwe hawawezi kuja wenyewe, ni lazima waone ili
wajue unachofanya. Unaweza kuweka bango mbele ya biashar ayko, ukiweza
kuweka bango lenye taa ni vizuri kwani hutangaza biashara yako hata
wakati wa usiku. Unaweza kutangaza biashara yako kwenye majarida au
mitandao mbali mbali. Njia nyingine nzuri ni kutengezena tovuti nzuri ya
biashara yako, inayoweza kufunguka vizuri kwenye simu kwa sababu siku
hizi watu wengi hutumia simu za mkononi kutafuta bidhaa na vitu mbali
mbali wanvyohitaji. Hivyo unaweza kupata mtaalamu wa kukutengezea tovuti
na kuisanifu vizuri ili iweze kupatikana kirahisi kwenye mtandao haswaa
mtu anapo ‘Google’. Unaweza pja kutumia mitandao ya kijamii kutangaza
biashara yako kwa kuwashirikisha watu uliojiunga nao kwenye matando
wako.
- Weka malengo kwenye biashara yako.
Je unahitaji kuwa na duka ligine ifikapo mwakani au kufungua tawi la
bishara yako nchi jirani baada ya miaka mitano au kufikia mauzo ya
milioni 50 kwa mwaka ndani ya mwaka mmoja. Ni muhimu kuyaandaka malengo
yako ili yaweze kukongoza kuhusu ni ni ufanye na nini usifanye kwenye
biashara yako. Pia yatakuongoza kuamua kiasi cha mtajim kinachohitajika
pamoja na aina ya watu utakaohitaji kufanya nao kazi.
- Fungua akaunti ya benki.
Kitu cha muhimu kuzingatia katika biashara yako ni namna unavyoweza
kusimamia mapato na matumizi yako. Biashara nyingi hushindwa kuendelea
kutokana na wamiliki kushindwa kusimamia vizuri fedha za biashara.
Unatakiwa kukusanya mapato yako mapema iikiwezekana wateja walipie
kwanza, ila watu wanokudai wantakiwa walipwe mwishoni ili kuhakikisha
kuwa biashara inakuwa na fedha za kujiendesha wakati wote. Njia nzuri ya
kutunza feedha ni kuwa na akaunti za benki, akaunti ya kufanyia na
kupokea malipo na akaunti ya kutunzia fedha unaweza mkuwa na akaunti
zaidi ya moja za kutunza fedha. BancABC ni benki inayotoa huduma nzuri
zaidi kwa wanya bishara wadogo wadogo.
No comments:
Post a Comment