Thursday, 25 August 2016

SAMATTA AIPELEKA GENK MAKUNDI EUROPA


samatta

Mbwana Samatta amezidi kung’aa baada ya kuifungia timu yake ya KRC Genk bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia na kufuzu moja kwa moja kucheza hatua ya makundi ya Michuano ya Europa.

Katika mchezo huo ulofanyika kwenye dimba la Cristal Arena maskani mwa Genk, Samatta ndiye alifungua ukurasa wa mabao kwa Genk baada ya kufunga goli mnamo dakika ya kwanza lilitokana na shuti kali kufuatia pasi nzuri kutoka kwa Leon Bailey.
Genk walienda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja kwa bila.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Genk wakifanya jitihada za kutafuta bao lingine, na ndipo Leon Bailey alipoiandikia Genk bao la pili dakika ya 50 kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Leandro Trossard na kuifanya Genk kufuzu kwa wastani wa mabao 4-2.
Baada ya mchezo wa leo, Genk sasa inaungana na vigogo kama kama Manchester United, Fenerbahce na wengine kucheza katika hatua ya makundi ya Europa.
Kikosi cha KRC Genk : Bizot, Walsh, Dewaest, Colley, Uronen, Heynen, Ndidi, Pozuelo (81 ‘Kumordzi) Bailly (73’ Kebano) Trossard and Samatta (79 ‘Karelis).
Kikosi cha NK Lokomotiva : Zagorac, Bartolec, Rozman, Maric, Fiolic, Peric, Grezda (45 ‘Coric), Sunjic, Capan (65’ Ivanusec) Bockaj (72 ‘çekici) and Majstorovic.
Magoli :
02 ‘: 1-0: Samatta
50’: 2-0: Bailey
Kadi za njano : 42 ‘Rozman, 64’ Capan, 69 ‘Samatta, 80’ Bizot
Nyekundu: 0
Mwamuzi: John Beaton (Scotland)
Mahudhurio : 8,540

No comments:

Post a Comment