| Venance Mwamoto |
MBUNGE
wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Venance Mwamoto
amewataka walimu wakuu wa shule na kamati za
shule wilayani humo kuhakikisha
wanapokea madawati yenye kiwango kinachotakiwa.
Mwamoto
ameyasema hayo wakati akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Idegenda wakati na
kuongeza kuwa mfuko wa Jimbo ulitoa shilingi milioni 30 kwa
ajili ya kutengeneza madawati 600 ili kumaliza
tatizo la uhaba wa madawati katika wilaya ya
Kilolo.
Amesema
lengo la kutoa pesa hizo ni kuona madawati
yanayotengenezwa yanakuwa na kiwango kizuri ili wanafunzi
waweze kuyatumia kwa muda mrefu na sio
kuendelea kutengeneza madawati kila mwaka.
Amesema
pesa hizo ni za wananchi wa Kilolo hivyo hajakubaiana na kiwango cha
ubora wa madawati hayo na kulazimika kuyakataa madawati hayo
na tayari mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina
Masenza naye ameyakataa madawati hayo 745 na mengine ambayo idadi yake
inafika zaidi ya madawati 10000
Nao
uongozi wa shule ya Msingi Idegenda umemweleza
mbunge huyo katika mkutano huo kuwa
madawati zaidi ya 200 ambayo shule hiyo imepokea
hayana ubora na hivyo walichokifanya ili kuepuka
kuwajibika kwa kushindwa kusimamia madawati hayo
wamelazimika kuchagua madawati yote mabovu na kuyahifadhi stoo
.
No comments:
Post a Comment