BARAZA la Mitihani nchini (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita (ACSEE) ambayo pamoja na mambo mengine yanaonesha wasichana wanaongoza kwa ufaulu wa asilimia 98.59 dhidi ya wavulana ambao wamefaulu kwa kiwango cha asilimia 97.55.
Matokeo hayo yanaonesha kuwa kati ya wasichana 27,717 walioandikishwa kufanya mtihani huo 26,977 wamefaulu na waliofeli wakiwa 740.
Kwa upande wa wavulana kati ya 47,179 walioandikishwa kufanya mtihani huo waliofeli ni 2,605 wakati waliofaulu wakiwa 44,574.
Licha ya matokeo hayo kuonesha wasichana wengi wamefaulu, hata hivyo wavulana ndio wanaongoza katika ufaulu wa somo la sayansi kwa kushika nafasi nane kati ya kumi bora huku wasichana wakiwa wawili pekee.
Matokeo hayo yalitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde, katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo hayo ambayo yamechakatwa kwa kutumia mfumo wa ‘division’, baadhi ya shule kongwe za Serikali ambazo katika miaka ya hivi karibuni zilionekana kufanya vibaya na hivyo kufuta rekodi nzuri ilizoziweka miaka ya nyuma, zimeonekana kurudi katika chati ya kumi bora ikiwamo Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora, Kibaha, Mzumbe na Ilboru.
Shule ya wavulana Tabora imeongoza kwa kutoa mwanafunzi wa kwanza bora katika somo la sayansi ambaye ni Hassan Gwaay, aliyekuwa akichukua mchepuo wa PCM.
Shule ya Sekondari Tandahimba ya mkoani Mtwara nayo imeonekana kuchomoza katika orodha ya shule kumi bora kitaifa ikitanguliwa na Kisimiri ambayo imeshika nafasi ya kwanza, Feza Boys (2), Alliance Girls (3), Feza Girls (4), Tabora Boys (5), Marian Boys (6), Kibaha (7), Mzumbe (8) na Ilboru (9).
Lakini wakati shule hizo ziking’ara, shule kongwe ya Serikali ya Azania iliyoko Dar es Salaam imeanguka vibaya katika matokeo hayo kwa kushika nafasi ya tisa kati ya kumi kwenye orodha ya shule zilizofanya vibaya.
Katika orodha hiyo, shule saba za sekondari zilizoko Unguja visiwani Zanzibar ambazo ni Mpendae, Ben Bella, Tumekuja, Jang’ombe, Kiembesamaki, Al-Ihsan Girl’s na Lumumba nazo zimefanya vibaya pamoja na Green Bird Boys ya Kilimanjaro.

No comments:
Post a Comment