Kundi la wapiganaji wa Islamic State wametoa madai kupitia mtandao wao unao julikana kama Amaq, kuwa wao ndio walio husika katika shambulio lililofanywa na mwanachama wao ambae aliwakanyaga watu na loli.
IS wamekuwa wakitumia mtandao wa Amaq kueneza propaganda zao.
Hata hivyo hakuna habari za kuthibitisha kuwa kundi hilo lilihusika moja kwa moja na shambulio hilo.
Tovuti hiyo ya Amaq imekuwa ikieneza taarifa ya IS inayohimiza waislamu kushambulia mtu au watu wanaotoka nchi za muungano wa mataifa yanayoshambulia kundi hilo.
Hata hivyo kuna wanaosema IS imetumia nafasi ya shambulio hilo kujikuza ingawa huenda kamwe hawakuhusika.

No comments:
Post a Comment