VIDEO:50 Cent akamatwa na polisi baada ya kutamka neno “M*therfucker” akiwa stejini.
Rapper asieishiwa vituko na matukio Curtis Jackson a.k.a 50 Cent,alfajiri
ya kuamkia June 27 alijikuta akiwa mikononi mwa polisi,akishikiliwa kwa
kosa la kutamka lugha ya matusi mbele ya hadhira wakati aki-perfom
kwenye mji wa St.Kitts,uliopo pwani ya visiwa vya Caribbean weekend hii. Inadaiwa
kuwa 50 Cent,alitaamka neno “motherf*cker,”wakati aki-perfom wimbo wake
wa ‘P.I.M.P’ akiwa ameshika kipaza sauti huku akijua wazi kuwa DJ wake
hakuwa na ‘clean version’ (mashairi yaliyohaririwa) ya wimbo huo.
Hata hivyo rapper huyo aliruhusiwa kumaliza show yake,ambapo
iliwabidi polisi wamsubiri ashuke stejini huku taarifa za awali zikidai
kuwa kutokana na kitendo hicho atakabiliwa na mashtaka ya utovu wa
nidhamu ‘misdemeanor charge’.
Hatua hii inaweza kuwa funzo kwa wanamuziki wengine hata hapa
nyumbani,hasa wale wanaopenda kutoa lugha za matusi au zenye kuudhi
wakiwa stejini bila kujali mashabiki wao wanaathirika kiasi gani na
matamshi ya aina hiyo.
No comments:
Post a Comment