Wednesday, 15 June 2016

Utajuaje kama rafiki/mpenzi wako anakutumia ?

Kuna aina mbalimbali za watu tunakutana nao katika maisha yetu, na sio kila anaekuwa karibu na wewe, anakujali au anakupenda wapo walio kimaslahi zaidi, na sio lazima iwe pesa,inaweza ikawa hata jinsi mtu anavyotumia muda wako bila kujali wewe umeacha vingapi uwe na yeye.
Lakini utajuaje kama mtu anakutumia, hizi ni ishara zake,
Anakutafuta akiwa na shida tu
Ukiona una mpenzi/Rafiki Hakupigii simu wala kukujulia hali kipindi chochote mpaka awe na shida zake huyo anakutumia, kama ni mwanaume anakutafuta akiwa tu anataka ngono na wewe au  kama mwanamke anakutafuta tu akiwa amekwama anataka pesa huyo anakutumia.
Hakosi Dharura
Ukiwa na rafiki/mpenzi ambaye kila siku ukiwa unamuhitaji au kama unataka kuonana nae, anakwambia yuko na kazi nyingi ofisini Mara hawezi kukuona  ana mikutano mara katoka na marafiki, aina ya watu ambao kuonana na wewe lazima apate kisingizio mtu wa aina hiyo anakutumia tu.
Anakuazima Vitu na Harudishi
Kila siku ni mtu wa kuomba vitu kwako, mara flash disk mara kaomba earphone, au anakuazima pesa ambazo harudishi,  mtu wa aina hii kila siku anakuomba vitu na harudishi huyo ni mtu anaekutumia tu, anakuagiza sehemu ambazo anajua yeye hana muda wa kwenda ila anataka wewe umsaidie bila kujali unafanya nini kwa wakati huo.
Hakusikilizi
Ukiwa nae karibu yuko karibu na simu yake au kazi zake kwenye komputa yake na hana muda na wewe, ukiongea angalia ni kwa kiasi gani anakusikiliza mawazo yako , kama ni mtu asiye thamini muda wako au uwepo wako huyo mtu lazima anakutumia. akiwa karibu na watu wake au marafiki zake anajidai hakuoni au hama muda na wewe,
Hajali Matatizo Yako
Unapokuwa na matatizo, hajalihayupo na wewe wakati wote unao muhitaji karibu, ila ni yeye anaekutafuta kila napokuwa na matatizo uyake basi anakutumia.

No comments:

Post a Comment