Tuesday, 21 June 2016

REAL MADRID KUTUMIA TRUFU KUWAPIKU ARSENAL NA CHELSEA KUMNUNUA ALVARO MORATA TOKA JUVENTUS!


REAL-MORATAMadrid wanatarajiwa kutumia Kipengele cha Mkataba wa Alvaro Morata ili wamsaini tena Mchezaji wao wa zamani kwa mujibu wa Mkuu wa Klabu ya Juventus Giuseppe Marotta.
Morata ambae alitamba na Juve Msimu uliopita alipowawezesha kutwaa Ubingwa wa Serie huko Italy kwa mara ya 5 mfululizo na sasa anang’ara huko France kwenye EURO 2016 akiwa na Spain na Juzi kuifungia Bao 2 walipoichapa Turkey.
Straika huyo ameleta mvuto mkubwa huko Ulaya na Klabu za Ligi Kuu England, Arsenal na Chelsea, ni miongoni mwa zile zinazotajwa kumuwinda.
Mkuu wa Juve, Giuseppe Marotta, amethibitisha kuwa Morata ataondoka na anaweza kurudi Real Madrid ambako aliuzwa kwa Juve Mwaka 2014 kwani Mkataba wa Mauzo yake una Kipengele cha Kumnunua tena kwa Euro Milioni 30.
Giuseppe Marotta amesema sasa wanachosubiri ni Ofay a Maandishi kutoka Real na ndipo watajua nini cha kufanya ingawa amekiri hawana njia ya kumzuia Morata.
Morata aliondoka Santiago Bernabeu Mwaka 2014 baada ya kukaa hapo kwa Miaka 6 ambako alianzia Timu ya Vijana Mwaka 2008 akitokea Getafe na kabla alikuwa na Atletico Madrid kuanzia 2005.
Akiwa na Real, Morata aliichezea Timu ya Kwanza mara 37 na kufunga Bao 10.

No comments:

Post a Comment