SAFU ya Robo Fainali ya UEFA EURO 2016, Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, imekamilika Jana baada ya Italy na Iceland kushinda Mechi zao.
Ifuatayo ni Ripoti kuhusu Timu hizo 8 zilizotinga Robo Fainali inayogusa Rekodi zao kwenye EURO na pia njia waliyopita kuingia hatua hii.
RIPOTI YA TIMU 8 ZILIZOINGIA ROBO FAINALI:
**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za Bongo
Alhamisi: Poland v Portugal, Marseille
Poland
EURO-Rekodi Bora: Robo Fainali Mwaka 2016
Robo Fainali-Rekodi: Robo Fainali Mwaka 2016
Njia kutua Robo Fainali: 1-0 Northern Ireland, 0-0 Germany, 1-0 Ukraine, 1-1 Switzerland (Penati 5-4)
Takwimu muhimu: Robert Lewandowski hajafunga Bao katika Mechi 7 zilizopita akichezea Poland.
Portugal
EURO-Rekodi Bora: Mshindi wa Pili Mwaka 2004
Robo Fainali-Rekodi: W3 L2
Robo Fainali-Mara yao ya mwisho: 1-0 Czech Republic, 2012
Njia kutua Robo Fainali: 1-1 Iceland, 0-0 Austria, 3-3 Hungary, 1-0 Croatia
Takwimu muhimu: Cristiano Ronaldo amebakiza Bao 1 tu kuishika Rekodi ya Michel Platini ya Ufungaji Bora kwenye Fainali za EURO akiwa na Bao 9.
Ijumaa: Wales v Belgium, Lille
Wales
EURO-Rekodi Bora: Robo Fainali Mwaka2016
Robo Fainali-Rekodi: Robo Fainali Mwaka2016
Njia kutua Robo Fainali: 2-1 Slovakia, 1-2 England, 3-0 Russia, 1-0 Northern Ireland
Takwimu muhimu: Wales wametinga Robo Fainali yao ya kwanza ya Mashindano makubwa kwa mara ya kwanza tangu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1958.
Belgium
EURO-Rekodi Bora: Mshindi wa Pili Mwaka 1980
Robo Fainali-Rekodi: Mshindi wa Pili Mwaka 1980
Njia kutua Robo Fainali: 0-2 Italy, 3-0 Republic of Ireland, 1-0 Sweden, 4-0 Hungary
Takwimu muhimu: Belgium wamejaribu Mashuti 84 Golini wakizipta Timu zote kwenye EURO 2016.
Jumamosi: Germany v Italy, Bordeaux
Germany
EURO-Rekodi Bora: Mabingwa (1972, 1980, 1996)
Robo Fainali-Rekodi: W3 L0
Robo Fainali yao ya mwisho: 4-2 Greece, 2012
Njia kutua Robo Fainali: 2-0 Ukraine, 0-0 Poland, 1-0 Northern Ireland, 3-0 Slovakia
Takwimu muhimu: Chini ya Kocha Joachim Löw, Germany hawajafungwa hata Bao 1 kwenye Fainali hizi za EURO 2016.
Italy
EURO-Rekodi Bora: Mabingwa (1968)
Robo Fainali-Rekodi: W2 L1
Robo Fainali yao ya mwisho: 0-0 (Walishnda kwa Penati 4-2) England, 2012
Njia kutua Robo Fainali: 2-0 Belgium, 1-0 Sweden, 0-1 Republic of Ireland, 2-0 Spain
Takwimu muhimu: Italy waliifunga Spain Juzi kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EURO 2016 na kuwa Timu ya kwanza kuitoa Spain kwenye Raundi za Mtoano za Fainali ya Mashindano makubwa tangu 2006.
Jumapili: France v Iceland, Saint-Denis
France
EURO-Rekodi Bora: Mabingwa (1984, 2000)
Robo Fainali-Rekodi: W2 L2
Robo Fainali yao ya mwisho: 0-2 Spain, 2012
Njia kutua Robo Fainali: 2-1 Romania, 2-0 Albania, 0-0 Switzerland, 2-1 Republic of Ireland
Takwimu muhimu: France (1984) ni moja ya Timu 3 kutwaa EURO wakiwa Wenyeji na wanaungana na Spain (1964) na Italy (1968) waliowahi kufanya hivyo.
Iceland
EURO-Rekodi Bora: Robo Fainali Mwaka 2016
Robo Fainali-Rekodi: Robo Fainali Mwaka 2016
Njia kutua Robo Fainali: 1-1 Portugal, 1-1 Hungary, 2-1 Austria, 2-1 England
Takwimu muhimu: Wakiwa na Idadi ya Watu 330,000, Iceland ndio Nchi ndogo kabisa kucheza Fainali za Mashindano makubwa.
No comments:
Post a Comment