Mji wa Hong Kong
ndio mji ghali zaidi duniani baada ya kuupiku mji wa Luanda, Angola
kulingana na wafanyikazi wa kimataifa katika utafiti wa kila mwaka
unaofanywa na shirika la Mercer.
Luanda ambao ulikuwa unaongoza orodha hiyo katika siku za hivi karibuni ulishuka kufuatia kudhoofika kwa sarufi yake.
Mji wa Luanda
Mji wa Zurich na Singapore ni ya tatu na nne mtawalia katika orodha hiyo ikiwa haijabadilika kwa mwaka mmoja sasa.
Mji wa Tokyo sasa umepanda hadi nafasi ya tano.
Zurich
Utafiti huo unalenga kampuni zinazotakiwa kuhesabu marupurupu ya wafanyikazi wa kimataifa.
Singapore
Umepima gharama ya kuishi kwa takriban mataifa 209
duniani,ikilinganisha gharama ya viti 200 katika kila eneo ikiwemo,bei
ya nyumba ya kuishi,uchukuzi,chakula na burudani.
No comments:
Post a Comment