Mbinu za polisi wakati wa maandamano dhidi ya sheria ya kazi Alhamisi Mei 26 katika mji wa Paris zimeibua maswali mengi.
Mamia ya
watu waliojificha nyuso zao, leo Jumanne wamekabiliana na vikosi vya
usalama, huku wakirusha mawe na vilipuzi wakati wa maandamanao
yaliyofanyika mjini Paris dhidi ya sheria ya kazi.
Watu kumi
na tatu walmekamatwa, polisi katika mji wa Paris (PP) imesem. Kwenye
akaunti yake ya Twitter, polisi imetoa wito kwa waandamanaji kuajitenga
na makundi ya wahuni, ili kuwezesha kuingilia kati kwa vikosi vya
usalama.
Katika
eneo la Port-Royal, "watu waliingia katika jengo moja ambalo bado
linajengwa na kuchukua vifaa vya ujenzi ambavyo walivitumia kwa kurushia
vikosi vya usalama, ambavyo vililazimika kuingilia kati", polisi ya
mjini Paris imesema.
Polisi
wametumia mabomu ya machozi na kuwatimuwa waandamanaji ambao wamekua
wakirusha vilipuzi huku wakipiga kelele wakisema "wakazi wa mji wa
Paris, simameni, inukeni!" au "kila mtu aichukie polisi". hali hiyo
inatokea siku moja baada ya kifo cha askari polisi na mpenzi wake karibu
na mji wa Paris katika shambulio la wanajihadi.
Kwa uchache watu wawili wamejeruhiwa, mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP, ameshuhudia.
Vio vya madirisha kadhaa vya benki vimevunjwa na wahuni wakati mwingine wakiungwa mkono na baadhi ya waandamanaji.
No comments:
Post a Comment