Tuesday, 21 June 2016

Akon kutunukiwa tuzo ya heshima aliyopewa Millen Magese mwaka jana na BET Awards

Mwanamuziki na Mwanaharakati Akon atatunukiwa tuzo ya heshima ya  Global Good ya BET Awards 2016.
Akon_4_Africa
Akon atapewa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kuleta maendeleo kupitia mradi wake wa kusambaza umeme wa Solar kwa waafrika Akon Lighting Africa, uliosaidia watu zaidi ya Million 600 kwenye nchi zaidi ya 11 za Afrika hadi sasa.
Tuzo hiyo ambayo imeanza kutolewa Mwaka jana kwa watu ambao wanamchango mkubwa kwenye kuleta maendeleo ya waafrika, mwaka jana alipewa mwanamitindo na Miss Tanzania, 2001, Happiness Millen Magese.

No comments:

Post a Comment