Wednesday, 25 May 2016

WACHEZAJI 9 WENYE ELIMU KUBWA ZAIDI DUNIANI

Van der Sar


Na Mahmoud Rajab
Imezoeleka sana hapa Tanzania na pengine duniani kwa ujumla kuona vijana wengi wenye vipaji vya soka kuachana na masomo na kukimbilia kucheza soka.
Wengi wao huishia shule za msingi na angalau kidogo wengine hufika hadi sekondari.
Licha ya waachezaji wengi kujengwa na ‘mentality’ hiyo lakini kuna wengine ambao kwa upande wao huwa wanapiga kote kote yaani shule pamoja na soka.
Kwa uchache tu angalia orodha hii ya wachezaji ambao wamewahi kuwa na kiwango cha juu kabisa cha elimu duniani kuliko wengine ambayo imeripotiwa na mtandao wa sokkaa.com.
  1. Simon Mignolet -Shahada ya masuala ya Sheria

Huyu ni mlinda lango wa Liverpool. Mignolet ana Shahada ya masuala ya Sheria na Sayansi ya Kisiasa aliyoipata kwenye Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Leuven (Catholic University of Leuven) kilichopo Ubelgiji. Anaweza kuzungumza lugha nne kwa ufasaha: Kiingereza, Kifaransa, Kiholanzi na Kijerumani.
  1. Shaka Hislop-Shahada ya Heshima ya uhandisi Magari
Huyu ni mlinda lango wa zamani wa Newcastle United. Amebobea katika masuala ya uhandisi wa magari. Alipata shahada yake ya uhandisi wa magari katika chuo kikuu cha Howard (Howard University). Kwa sasa, anatumika kama mchambuzi wa mambo ya soka kwenye ESPN.
  1. Iain Dowie-Shahada ya Uzamili katika Uhandisi
Mshambuliaji wa zamani wa Southampton, West Ham na QPR anamiliki Shahada ya Uzamili ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Hertfordshire (University Hertfordshire). Alijulikana pia kama mtu aliyetumika katika Kampuni ya Huduma za Anga nchini Uingereza(British Aerospace).
  1. Steve Coppell-Shahada katika Mambo ya Uchumi
Coppell alicheza Manchester United mwishoni mwa mwaka 1970 na mwanzoni mwa1980. Alipata Shahada katika Mambo ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Liverpool (University of Liverpool).
  1. Dennis Bergkamp-Shahada ya Uhandisi wa Kidaktari
Alipokuwa akicheza Arsenal, mshambuliaji huyo zamani wa wa Uholanzi alishinda Shahada katika Uhandisi wa Kidaktari kutoka University of Bath. Kwa sasa ni kocha msaidizi wa klabu ya Ajax Amsterdam.
  1. Barry Horne-Shahada ya masuala ya Kemia
Kiungo wa zamani wa Everton ni alihitimu Shahada ya Kemia katika Chuo Kikuu cha Liverpool. Anafundisha Kemia na Fizikia katika shule za sekondari jijini Chester ambapo hutumika pia kama Mkurugenzi wa Soka.
  1. David Wetherall-Daraja la kwanza la Shahada ya Heshima katika Kemia
Beki wa zamani wa Bradford city alipata wa Daraja la kwanza la Shahada ya Heshima katika Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield (University of Sheffield).
  1. Edwin van der Sar-Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Michezo 
Golikipa huyu wa zamani wa Manchester United alikuwa na mafanikio makubwa akiwa Old Trafford ambapo aliweza kushinda mataji mengi kukiwemo Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu ya England.
Hivi karibuni alikamilisha Shahada yake ya Uzamili ya kimataifa katika Uongozi wa Michezo. Sasa anatumika kama Mkurugenzi wa Masoko katika klabu ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi.
  1. Socrates-Shahada ya udaktari katika Tiba
Socrates alizaliwa mnamo 1954 huko Belém, Para (Brazil) na alifariki dunia mnamo 2011 akiwa na umri wa miaka 57. Licha ya kuwa hodari zaidi katika soka, huyu ndiye anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyewahi kuwa na elimu kubwa zaidi ulimwenguni.
Alikuwa daktari tiba na alikuwa anamiliki wa Shahada ya Falsafa (PhD).

Comments

No comments:

Post a Comment