Mchezo wa soka unatajwa kuwa ni mchezo wa urafiki, undugu na wakiungwana. Hata hivyo wapo wachezaji ambao wanacheza tofauti na hivyo na kujikuta wakiadhibiwa kwa kadi au wakati mwingine hata kufungiwa kabisa kutokana na vitendo vyao vichafu dhidi ya wenzao, waamuzi, mashabiki na hata viongozi.
Lakini pia wapo wachezaji ambao wanacheza kwa kufuata kanuni na sheria zianazotawala mchezo husika na kuweka historia. Kwa bahati mbaya mchezaji kama Lionel Messi hayupo kwenye orodha kama hii kutokana na Mu-Argentina huyo kuoneshwa kadi nyekundu kwenye maisha yake ya soka.
Hawa ni wachezaji nane ambao hawajawahi kuoneshwa kadi nyekundu kwenye maisha yao ya kusakata soka.
8. Luke Young
7. Ledley King
Kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa kati kucheza maisha yote bila kuoneshwa kadi nyekundu inahitaji kichwa kilichotulia wakati wa kufanya maamuzi na wakati mwingine huenda ikawa ni bahati. Timing mbovu au kiwiko kinaweza kukufanya uingingie kwenye kitabu cha kichafu cha waamuzi.
6. Damien Duff
Huyu Mu-Irish ameingia kwenye orodha hii akiwa na tofauti kubwa katika ngazi zote kitaifa na kimataifa. Katika miaka yake yote ya kucheza soka, hajawahi kuoneshwa kadi nyekundu na anaendelea kucheza soka hadi sasa katika klabu ya Melbourne FC. Amestaafu soka la kimataifa miaka miwili iliyopita.
5. Raul Gonzalez
Mkongwe wa Hispania ni miongoni mwa wachezaji waliowahi kuwa wasafi katika historia ya soka. Katika maisha yake marefu ya soka akifanikiwa kucheza michuano mbalimbali ya kombe la dunia pamoja na kucheza michuano yenye tension kubwa kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid lakini bado hakuwahi kuoneshwa kadi nyekundu.
Haya ni mafanikio makubwa kwake kwenye historia ya maisha yake ya soka.
4. Ryan Giggs
Watu wengi wanamtambua raia huyu wa Wales kutokana na uwezo wake mkubwa uwanjani. Alistaafu soka mwaka 2014 baada ya kuitumikia Manchester United kwa maisha yake yote akiwa kama mchezaji na kwasasa ni kocha msaidizi pale Old Trafford.
Ryan Giggs ameshiriki kwenye kila kila msimu wa ligi tangu 1990 hadi 2014, na ni miongoni mwa wachezaji wenye mafanikio ndani ya Premier League. Licha ya kucheza kwa kutumia nguvu lakini bado Giggs ni miongoni mwa wachezaji ambao hawajawahi kukutana na kadi nyekundu kwenye maisha yao yote ya uchezaji soka.
3. Gary Lineker
Gary Lineker alitamba na timu ya taifa ya England ‘the lions’ kwenye kombe la dunia nchini Italy mwaka 1990. Akicheza sambamba na Paul Gascoigne alikuwa na jukumu la kuwaweka wachezaji wenzake kwenye mstari mnyoofu na kuhakikisha mawazo yao yanakuwa kwenye mchezo.
2. Edwin Van Der Saar
Golikipa wa zamani wa Uholanzi amekuwa ni miongoni mwa wachezaji wa kidachi wenye mafanikio makubwa kwenye ligi ya England.
Na alipokuwa akiokoa michomo na kuisaidia timu yake kupata ushindi, nidhamu yake bado bado ilikuwa ni ya juu.
Amecheza zaidi ya dakika 27,000 akiitumikia Manchester United na hajaoneshwa kadi nyekundu katika muda wote huo.
1. Alessandro Del Piero
Alessandro Del Piero maisha yake ya soka ya zaidi ya miongo miwili (1991 hadi 2014) yanashangaza, mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 2006 alikuwa ni mwenye kasi, tackle za akili nyingi na kichwa kilichotulia alimaliza maisha yake ya soka bila kuoneshwa kadi nyekundu hata moja.
No comments:
Post a Comment