Mgombea uteuzi wa urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump, amepata kura za kutosha kutoka wajumbe wa chama hicho kuweza kusimama kama mgombea. Bilionea huyo, ambaye ndiye mgombea pekee aliyesalia kwenye kinyang'anyiro cha chama chake, anatamiwa kukubali uteuzi kwenye mkutano mkuu wa Republican mjini Cleveland. Hivi leo, akiwa kwenye mkutano wa mataifa saba yenye nguvu za viwanda duniani, G7, Rais Barack Obama alisema viongozi wenzake wa dunia wanashangazwa na baadhi ya sera za Trump, ambazo zinaonesha namna kiongozi huyo asivyoelewa ulimwengu unavyofanya kazi. Akizungumza na waandishi wa habari kandoni mwa mkutano huo, unaoendelea nchini Japan, Obama amesema viongozi wenzake hawana hakika na umakini wa mgombea huyo. Trump, bilionea wa biashara ya majengo na mwendeshaji wa kipindi cha televisheni, amevutia vichwa vya habari tangu azinduwe kampeni yake ya kuwania urais mwaka jana, akiwa na kauli zinazoonekana kuwavunjia heshima jamii za Waislamu, Wamexico na wanawake, miongoni mwa wengine wengi.
Thursday, 26 May 2016
Trump apata kura za kutosha kugombea urais

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment