May 22 2016 headlines kwa upande wa wapenda soka Tanzania ilikuwa ni habari kuhusu soka la Tanga, ambapo leo haikuwa siku nzuri kwa wapenda soka la mkoa huo, May 22 ndio siku rasmi soka la Tanga limepata bahati mbaya ya kushusha timu tatu Ligi Kuu.
Baada ya Coastal Union na African Sports kushuka daraja, klabu ya Mgambo JKT
ambayo awali ndio ilikuwa na matumaini ya kufanya vizuri na kubakia
Ligi Kuu, leo imeshuka daraja rasmi baada ya kutoka sare ya goli 1-1
dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Azam Complex.
Sare dhidi ya Azam FC imeifanya Mgambo JKT
kufikisha jumla ya point 28 huku ikiwa katika nafasi ya 14 katika
msimamo wa Ligi Kuu, kwa mujibu wa sheria ya Ligi Kuu ni kuwa timu tatu
za mwisho huwa zinashuka daraja, kwa maana hiyo Coastal Union, Mgambo JKT na African Sports ndio zinakuwa timu tatu kutoka mkoa mmoja kushuka daraja.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa leo May 22 2016
- Simba 1-2 JKT Ruvu
- Majimaji 2-2 Yanga
- Mwadui FC 0-2 Kagera Sugar
- Toto Africans 0-1 Stand United
- Mtibwa Sugar 2-0 Africans Sports
- Mbeya City 0-0 Ndanda FC
- Tanzania Prisons 2-0 Coastal Union
No comments:
Post a Comment