Uongozi wa Azam FC leo May 23 2016 umeweka wazi mambo kadhaa kuhusu klabu hiyo, Azam FC kupitia kwa afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba aliweka wazi mambo kadhaa katika mkutano na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kuinua soka la vijana.
Katika mkutano huo Saad Kawemba akiwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Sheikh Said Muhammad aliweka
wazi mpango wao wa kuendeleza soka la vijana kwa utaratibu maalum. Mtu
wangu wa nguvu naomba nikusogezee mambo matatu waliozungumza Azam FC leo May 23 2016.
- Kwanza ni mpango wao wa kuinua soka la vijana, kwani baada ya kufanya utafiti wameanzisha mashindano maalum ya vijana yatakayoanza May 31 katika uwanja wa Chamazi, kwa kushirikisha timu za Academy nne kutoka Kenya, Uganda na Tanzania kutoa mbili.
- Kama ulikuwa unajua Azam FC kunyang’anywa point tatu wamepoteza kwa sababu Ligi imeisha, basi utakuwa unakosea hata kama point zao wakirudishiwa hawatopata Ubingwa lakini wamekata rufaa kwa ajili ya kuweka takwimu zao sahihi.
- Kuhusu Farid Musa aliyekuwa Hispania, amerejea Dar es Salaam na kweli amefanikiwa kufuzu majaribio katika klabu ya Deportive Tenerife ila bado mazungumzo yanaendelea na bado hawajafikia muafaka.
No comments:
Post a Comment