Real Madrid wametwaa taji la ubingwa wa vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya 11 baada ya kuichapa Atletico Madrid kwa mikwaju ya penati kwenye uwanja wa San Siro mjini Milan.
Bao la Sergio Ramos liliwaweka mbele vijana wa Zinedine Zidane kabla ya striker wa Atletico Antoine Griezmann hajakosa penati.
Mabadiliko yaliyofanywa na Diego Simeone kumuingiza Yannick Carrasco yaliupeleka mchezo huo extra time baada ya kuisawazishia timu yake kipindi cha pili.
Cristiano Ronaldo alipachika wavuni penati ya ushindi baada ya Juanfran kukosa penati yake kwa upande wa Atletico.
Mikwaju ya penati zilivyoamua matokea
Kwenye hatua ya mikwaju ya penati, Lucas Vazquez, Marcelo na Gareth Bale walifunga kwa upande wa Real, wakati Griezmann, Gabi na Saul Niguezwakijibu mapigo na kufanya matokeo ya penati kuwa 3-3.
Baada ya Ramos kuifungia Real mkwaju wan ne wa penati, na kufanya matokeo kuwa 4-3, Juanfran wa Atletico akagonshwa mwamba penati yake iliyokuwa ya nne kwa upande wa Atletico na kutoa nafasi kwa Ronaldo kushinda taji.
Mfungaji huyo bora wa muda wote wa mashindano akaizamisha wavuni penati yake na kufanikiwa kushinda taji la Champions League kwa mara ya tatu kama mchezaji binafsi kufuatia kutwaa taji hilo mwaka 2008 akiwa Manchester United, mwaka 2014 na 2016 akiwa na klabu ya Real Madrid.
Zidane amebebwa na mbinu zake
Zinedine Zidane alishinda Champions League akiwa kama mchezaji wa Real Mdrid mwaka 2002, amlichukua nafasi ya Rafael Benitez kama kocha mkuu mwezi January wakati huo Real ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 4-0 na Barcelona mwanzoni mwa msimu huku ikiwa kwenye hatihati ya kumaliza msimu wa pili bila taji lolote.
Akiwa na umri wa miaka 43, ameumaliza msimu akiwa kocha wa saba kuipa Real Madrid taji la Ulaya.
Aina yake ya uchezaji wa timu yake kwenye mchezo wa fainali, kadri kikosi chake kilivyokuwa kikishambulia walijitahidi kuwa imara zaidi katika eneo lao la ulinzi na kuwabana washambuliaji wa Atletico Griezmann pamoja na Fernando Torres hususan kipindi cha kwanza.
Gareth Bale na Ronaldo mara kadhaa walikuwa wakiruti katika eneo la katikati na kusaidia kuzuia mipira isiwafikie Griezmann naTorres, huku Karim Benzema pia akishuka chini kusaidia kukaba.
Atletico walirejea kwenye ubora wao baada ya mapumziko na kuongeza presha kubwa golini kwa Real iliyopelekea Pepe kumchezea vibaya Torres na hatimaye Atletico wakapata tuta huku Stefan Savic naye akipoteza nafasi ya dhahabu.
Nini kinamsibu Diego Simeona na Atletico?
Wiki tatu zilizopita Atletico walikuwa uwanjani wakicheza mechi ya ligi kujaribu kupambana kuona kama wanaweza kuufukuzia ubingwa wa La Liga, lakini kikosi cha Diego Simeone kimemaliza msimu huu kikiwa mikono mitupu baada ya kushindwa kutwaa ubingwa dakika za mwisho.
Wakiwa wamemaliza pointi tatu nyuma ya mabibwa wa La Liga FC Barcelona, wameachwa na maumivu tena kwenye fainali ya Champions League licha ya kuonesha kiwango cha hali ya juu katika kpindi cha pili ndani ya uwanja wa San Siro.
Griezmann aliendelea kuwa hatari kadri muda ulivyokuwa unasonga mbele, lakini kukosa kwake penati muhimu bado ilikuwa ni pigo kwa Atletico licha ya kwamba Carrasco baadaye aliisawazishia Atletico kwa kuunganisha krosi tamu ya Juanfran.
Ni mara ya tatu Atletico wamefika hatua ya fainali na kushindwa kulibakisha kombe. Simeone anatarajiwa kuendelea kukinoa kikosi cha Atletico kwa masimu ujao japo kuna vilabu vya England japo kuna vilabu vya Premier League vimeonesha nia ya kutahitaji huduma yake.
Kazi yake kubwa katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa ni kujaribu kuwabakisha nyota wake kama Griezmann, Saul Niguez ambao tayari wanahusishwa na vilabu vya Chelsea pamoja na Manchester United.
Clattenburg anastahili pongezi
Mwamuzi wa England Mark Clattenburg ametekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kuumudu mchezo wa derby ulioshuhudiwa kadi nane za njano zikitoka.
Beki wa Real Pepe alijaribu kumshawishi mwamuzi huyo wa EPL kufanya maamuzi ambayo yasingekuwa sahihi, lakini mwamuzi huyo pia alijaribu kumtuliza boss wa Atletico Madrid Diego Simeone baada ya Dani Carvajal kumchezea faulo Griezmann mapema kipindi cha kwanza.
Ramos aliipa goli la uongozi Real ambalo kwa namna flani lilikuwa likidhaniwa niwa ni la kuotea lakini msaidizi wa Clattenburg hakunyanyua kibendera na hiyo ilimaanisha lilikuwa goli halali.
Hata hivyo refa huyo ambaye pia yupo kwenye orodha ya waamuzi watakaochezesha michuano ya Euro 2016, alikuwa sahihi kutoa penati ambayo Griezmann alishindwa kuukwamisha mpira kambani kuisawazishia timu yake dakika ya 47.
Usipitwe na takwimu hizi muhimu
- Atletico sasa imekuwa ni klabu iliyofika mara nyingi (mara tatu) kwenye fainali ya European Cup/Champions League na kushindwa kutwaa taji hilo
- Hii ilikuwa ni fainali ya nane ya Champions League kufika hadi extra-time, nay a saba kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.
- Zinedine Zidane ni kocha wa pili (baada ya Miguel Munoz) kushinda la European Cup/Champions League akiwa kama mchezaji na baadaye kocha wa Real Madrid.
- Zinedine Zidane ni kocha wa kwanza kutoka Ufaransa kushinda Champions League.
- Sergio Ramos amekuwa mchezaji wa tano kufunga kwenye michezo miwili tofauti ya fainali ya Champions League huku akiwa beki wa kwanza kufanya hivyo (Raul, Samuel Eto’o, Lionel Messi and Cristiano Ronaldo).
- Ramos ameungana na Messi pamoja na Eto’o akiwa miongoni mwa wachezaji watatu kufunga magoli kwenye fainali zao mbili za kwanza za Champions League.
- Antoine Griezmann amekuwa mchezaji wa kwanza kukosa penati kabla ya zile za kutafuta mshindi kwa changamoto ya matuta. Mara ya mwisho Arjen Robben alifanya hivyo mwaka 2012 dhidi ya Chelsea.
- Marcello Lippi ndiye kocha aliyepoteza fainali nyingi za Champions League (tatu) akifatiwa na Diego Simeone (mbili).
No comments:
Post a Comment