Baada
ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
kueleza Bungeni kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
alijimilikisha ardhi iliyotolewa kwa wananchi wilayani Monduli mkoani
Arusha na kuahidi kuirejesha, Mwanasiasa huyo amejibu tuhuma hizo.
Lowassa amesema kuwa halijui shamba alilolizungumzia Waziri huyo na kwamba hakuna ardhi ambayo anaimiliki kinyume cha taratibu.
Alisema
kuwa hana taarifa kamili kuhusu maelezo ya Waziri Lukuvi na kwamba
ameomba Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (Chadema)
kulifuatilia kwa karibu na kumpa taarifa ili aweze kulitolea ufafanuzi.
“Nashindwa
kutoa maelezo kuhusu taarifa hizo kwa sababu sifahamu lolote kuhusu
shamba hilo,” Lowassa anakaririwa na gazeti la Jambo Leo lililofanya nae
mahojiano kwa njia ya simu.
“Mimi
sipo Bungeni, nimesikia hizo habari, lakini sijui zimetolewa lini na
nani. Mbunge wangu analifanyia kazi kwa sababu sina shamba
nilalolimiliki ambalo liko kinyume na taratibu,” aliongeza.
Akijibu
hoja ya Mbunge wa Monduli kuhusu umiliki na uporaji wa ardhi unaofanywa
na vigogo jimboni humo, Waziri Lukuvi alieleza kuwa kuna shamba ambalo
lilidhaminiwa na Rais Benjamin Mkapa ili wapewa wananchi jimboni humo,
lakini Lowassa alijimilikisha.
“Lile
Shamba la Makuyuni lilitolewa kwa wananchi litarudi kwao na ukae ukijua
litakuwa kwao kwa sababu aliyejimilikisha ni Edward Lowassa,” alisema
Lukuvi na kuahidi kulirejesha mikononi mwa wananchi hao.
No comments:
Post a Comment