Wednesday, 25 May 2016

Jay Z akana uvumi kuhusu ndoa yake na Beyonce

Jay Z na mkewe Beyonce

Nyota wa muziki wa Rap Jay Z hatimaye amezungumzia kuhusu uvumi unaozunguka ndoa yake na mkewe Beyonce.
Katika wimbo wake mpya Jay Z anasema kuwa ndoa yao ina thamani kubwa.
Mshororo huo kutoka kwa wimbo unaoitwa ,All the way up,ni jibu kwa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikizua uvumi kwa wiki kadhaa sasa kuhusu hatma ya ndoa ya wanamuziki hao wawili.
Uvumi huo ulianza kufuatia nyimbo katika albamu ya Beyonce ,Lemonade ambayo ilitaja uzinzi .Katika wimbo wake Sorry anaimba kwamba ''ananitaka wakati sipo.Afadhali amuite Becky mwenye nywele nzuri''.
Hatahivyo Beyonce anamuelezea Jay Z kama ''mume mzuri''.
Vilevile anasema kuwa ''angalia saa yangu,angekuwa nyumbani,leo najuta ile siku nilimvisha pete''.
Wengi walidhani kwamba Beyonce alikuwa akiimbia kuhusu maisha yake .
Lakini Jay Z amekana madai hayo katika wimbo huo mpya.Anasema kuwa 'Lemonade' ni kinywaji na kitasalia kuwa Kinywaji. 
Licha ya Beyonce kuimuimbia Jay Z kibao helo,wakati wa ufunguzi wa ziara yake ya muziki haikutosha kumaliza uvumi unaoendelea kati yao.
Alisema kuwa Jay Z ni mume mzuri na akawaambia mashabiki mjini Miami kwamba anampenda kwa dhati.

No comments:

Post a Comment