Leicester 1 Southampton 0
Man United 1 Everton 0
MANCHESTER UNITED Leo waliianza Siku kwa kulibatiza Jukwaa la Kusini la Old Trafford Jina la Lejendari wao Sir Bobby Charlton na kuliita Sir Bobby Charlton Stand na Wachezaji wa Timu hiyo hawakumuangusha pale waliposhinda Mechi yao ya Leo kwa Bao 1-0.
Katika Mechi hiyo ya BPL, Ligi Kuu England, Man United waliichapa Everton Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 54 la Anthony Martial alipounganisha Krosi ya Tineja Tim Fosu-Mensah.
+++++++++++++++++++++++++
REKODI-Man United wavunja rekodi ya Ligi Kuu England!
-Bao la Leo Anthony Martial ni la 1,000 kwenye BPL wakiwa Uwanjani kwao Old Trafford
-Arsenal inafuata kwa kufunga Bao nyingi kwao Emirates na Highbury=Bao 912
-Chelsea ni wa 3 kwa Bao 896
+++++++++++++++++++++++++
Ushindi huu umeipandisha Man United hadi Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Timu ya 4 Man City.
VIKOSI:
Manchester United: De Gea; Darmian, Smalling, Blind, Rojo; Schneiderlin, Carrick; Lingard, Mata, Martial; Rashford
Akiba: Romero, Fosu-Mensah, Valencia, Young, Fellaini, Herrera, Memphis
Everton: Joel; Baines, Jagielka (c), Stones, Coleman; Cleverley, McCarthy; Lennon, Barkley, Deulofeu; Lukaku
Akiba: Howard, Oviedo, Koné, Mirallas, Niasse, Besic, Funes Mori
REFA: Andre Marriner
No comments:
Post a Comment