Sunday, 3 April 2016

VPL: YANGA YASHINDA, YAWANYEMELEA SIMBA KILELENI, AZAM YANASA!





Ratiba:
Jumapili Aprili 3
Yanga 3 Kagera Sugar 1   
Toto Africans 1 Azam FC 1
Stand United 2 Mgambo JKT 0    
Ndanda FC 0 Tanzania Prisons 0  
JKT Ruvu 1 African Sports 0

Yanga, Mabingwa Watetezi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Leo wameitandika Kagera Sugar 3-1 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kuzidi kujichimbia Nafasi ya Pili na kuikaribia Simba kileleni.
Katika Mechi hii, Yanga walitanguliwa kufungwa kwa Bao la Mbaraka la Dakika ya 4 lakini wakaja juu na kupiga Bao kupitia Donald Ngoma, Dakika ya 25, Amisi Tambwe, 62, na Haji Mwinyi, 89.
Huko CCM Kirumba Jijini Mwanza, Azam FC waligonga mwamba walipobanwa na Toto Africans na kutoka Sare ya 1-1.
Azam FC walitangulia kufunga kwa Bao la John Boco la Dakika ya 23 na Toto kurudisha kwa Bao la Waziri Juma la Dakika ya 40.
Matokeo haya yanaibakisha Simba kileleni mwa VPL wakiwa na Pointi 57 kwa Mechi 24, Yanga wanafuata wakiwa na Pointi 53 kwa Mechi 22 na wa 3 ni Azam FC wenye Pointi 51 kwa Mechi 22.
LIGI KUU VODACOM  
MSIMAMO:
VPL-APR3                            
Ratiba:
Jumatano Aprili 6
Azam FC v Ndanda FC      
Majimaji v Coastal Union  

No comments:

Post a Comment