MASHABIKI wa Vinara wa BPL, Ligi Kuu England, Leicester City, Leo walipata burudani tosha baada ya Mmiliki wa Klabu hiyo kumpa kila mmoja wao aliehudhuria Mechi yao ya Leo ya Nyumbani kwao King Power Stadium waliyoifunga Southampton 1-0 Ofa ya Bia 1 na Andazi 1.
Ofa ya Bia ilikuwa kwa Watu wa Umri wa Miaka 18 kwenda juu na aliekuwa hakukidhi Umri huo alipewa Chupa ya Maji.
Ofa hii ilitolewa na Mmiliki wa Klabu hiyo, Vichai Srivaddhanaprabha, Raia wa Thailand ambae ni Tajiri mkubwa, ikiwa ni kusheherekea Siku yake ya Kuzaliwa ambayo ni Jumatatu.
Mashabiki hao walitakiwa wanywe Bia hizo nje ya Uwanja kabla ya Mechi.
Menejimenti ya Leicester imesema Mmiliki huyo ametoa Ofa hiyo ili kuwashukuru Mashabiki wote ikiwa ni kama shukrani yake kwao kwa sapoti kubwa Msimu huu wao wa mafanikio.
Baada ya Leo kuifunga Southampton 1-0 kwa Bao la Wes Morgan, Leicester wamepaa kileleni mwa BPL wakiwa Pointi 7 mbele ya Timu ya Pili Tottenham huku wakiwa wamebakisha Mechi 6 kumaliza Msimu.
Leicester wanaweza kutwaa Ubingwa wa England wakishinda Mechi zao 4 kati ya 6 walizobakisha.
LEICESTER CITY – Mechi zao za Ligi zilizobaki:
-Sunderland: 10 Aprili - Ugenini
-West Ham: 17 Aprili – Nyumbani
-Swansea: 24 Aprili - Nyumbani
-Manchester United: 1 Mei - Ugenini
-Everton: 7 Mei - Nyumbani
-Chelsea: 15 Mei - Ugenini
No comments:
Post a Comment