Monday, 7 March 2016

VAN GAAL ASHUSHA LAWAMA KWA WACHEZAJI WAWILI BAADA KIPIGO CHA WEST BROM (Video)

Louis




Louis van Gaal alikuwa katika siku mbaya tena jana baada ya timu yake kuchezea kichapo cha bao 1-0 mbele ya West Brom.
Van Gaal akaanza kutafuta namna ya kujitetea na ndipo akashusha zigo la lawama kwa kusema kadi nyekundu ya Juan Mata ilichangia timu yake kushindwa kupata matokeo ya ushindi. Kocha huyo wa kiholanzi amesema mwamuzi alipaswa kutazama namna ya kumwonya Mata kabla ya kumwonesha kadi ya pili ya njano.
Akiachana na habari za Mata, Van Gaal akaelekeza lawama zake kwa Anthony Martial akisema hakuwa katika ubora wake kwani alipiga shuti moja tu golini kwa dakika zote 90 alizocheza.
Lakini wakosoaji wamehoji kwamba, kama kinda huyo wa Ufaransa hakuwa kwenye ubora wake kwanini Van Gaal asingefanya mabadiliko ya kumpumzisha?

No comments:

Post a Comment