TFF imeagiza KRFA kuziagiza kamati zake kufanya uchunguzi juu ya matokeo ya mwisho katika mchezo kati ya Stand FC dhidi ya Kazima FC, ambapo Stand FC iliibuka na ushindi wa mabao 16 – 0.
Kabla ya mchezo huo wa mwisho, klabu ya Nyundo FC ilikuwa inaongoza kwa kuwa na pointi 21 na magoli 24 ya kufunga, na klabu ya Stand FC ilihitajia ushindi wa mabao 13 ili kuweza kuwa bingwa wa mkoa wa Katavi, hali inayopelea kuwepo kwa dalili za kupanga matokeo kwa ushindi wa Stand FC wa mabao 16 – 0 dhidi ya Kazima FC.
KRFA haitaruhusiwa kutangaza bingwa wa mkoa hadi uchunguzi ukamilke na TFF ijiridhishe na uchunguzi huo.
No comments:
Post a Comment