Polisi nchini Mali
wanasema watu wawili wamekamatwa kaskazini mwa nchi, kwa kuhusika na
shambulio lilofanywa mwezi huu na Al Qaeda, katika eneo la watalii
nchini Ivory Coast.
Mmoja wao anasemekana kuwa ndiye aliyepanga usafiri wa washambuliaji.Mwenzake anatuhumiwa kuwa mshauri mkuu kiongozi wa njama hiyo.
Wanaume wote wawili ni raia wa Mali.
Waliwapiga risasi waliokuwa wakikoga ufukweni, kabla ya kuivamia hoteli.
No comments:
Post a Comment