Tuesday, 22 March 2016

Ni kweli Ozil ataondoka Arsenal kwa sababu ya Wenger? ukweli wake huu

Kiungo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki anayekipiga katika klabu ya Arsenal ya Uingereza, kwa sasa jina lake limekuwa likitumika kuchochea tetesi za kuwa kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger huenda akafukuzwa kazi.
Jina la Ozil limeandikwa katika magazeti ya Uingereza kuwa hana furaha na kocha Arsene Wenger na yupo katika mchakato wa kuondoka kama kocha huyo ataendelea kubaki Arsenal, hivyo wengi kuanza kufikiria kuwa Wenger au Ozil, mmoja kati ya huenda ataondoka Arsenal.
12
“Nimeona ripoti nyingi leo katika vyombo vya habari, ukweli ni kuwa Arsene Wenger ndio sababu kubwa ya mimi kujiunga na Arsenal hilo bado halijabadilika” >>> Ozil
Maneno yamekuwa mengi sana, kitu ambacho kimemfanya Mesut Ozil kulazimika kutumia account yake ya twitter kuwa anafuraha na Wenger na ndio kocha aliyesababisha kujiunga na Arsenal.

No comments:

Post a Comment