Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amewasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi watano wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kutokana na uzembe unaodaiwa kusababisha kifo cha mama mzazi Pendo Masanja na watoto wake mapacha.
Tukio hilo linakuja ikiwa ni siku chache baada ya mapacha wengine
kupoteza maisha wakati wa kuzaliwa katika hospitali ya wilaya ya
nyamagana iliyopo Butimba jijini Mwanza kwa kile kinachoelezwa kuwa ni
uzembe wa wauguzi pamoja na madaktari wa hospitali hiyo kushindwa
kumhudumia kwa wakati mama mjamzito Suzan John machi 3 mwaka huu.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza pia amewasimamisha kazi wauguzi wengine
wawili wa hospitali ya Butimba ambao ni Nathan Bagaya na Edina
Mwesiga,Daktari mmoja wa Hospitali hiyo Furaha Kingunge na dereva wa
gari la kubeba wagonjwa ( AMBULANCE) Ghalib Hamad, huku akitangaza
kuunda tume ya watu wanne ikiongozwa na mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza
Dk. Onesmo Rwakyendera kwa ajili ya kuanza uchunguzi dhidi ya watumishi
hao.
Tume iliyoundwa na mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza kuchunguza uzembe wa
madaktari pamoja na watumishi wa hospitali hizo mbili za butimba na
Sekou Toure, huenda ikaja na majawabu sahihi na ufumbuzi wa changamoto
zinazopelekea kutokea kwa vifo vya watoto wachanga na akinamama
wajawazito wakati wa kujifungua.
No comments:
Post a Comment