Ukisikiliza simulizi za wanamuziki wengi,hawataacha kueleza changamoto na vikwazo walivyopitia katika harakati zao za kutoka kimuziki,achilia mbali kipaji,juhudi na uwezo binafsi ila kuna baadhi ya wasanii waliopata bahati ya kupewa support kwa namna ambayo iliwarahisishia kutimiza malengo yao ya kutoka kimuziki,hii hapa ni list ya mastaa kumi wa bongo fleva walitoka kimuziki kwa support ya wanamuziki wenzao.
10.DIAMOND & BOB JONIOUR.
Ni wazi kuwa Diamond Platnum ni miongoni mwa wanamuziki wenye mafanikio pengine kuliko wote Tanzania kwa sasa,ila hakuna asiyejua kuwa nyimbo zake za mwanzoni kuingia mainsteram kama “Kamwambie”,”Mbagala”ziliandaliwa chini ya Sharobaro Records ya Bob joniour,pengine Diamond alikua ana nyimbo nyingine alizorekodi kabla ya hizo ila nyimbo hizo mbili ndo ziliwafanya wengi wetu tumjue na kuanza kumfatilia Diamond.
Diamond Platnumz.
09.DOGO JANJA & MADEE.
Hakuna asiyejua kuwa Madee ndie mlezi wa kipaji cha rapper huyu kutoka Arusha ambae kwa sasa anatamba na hit song yake inayitwa “my life”.Achilia mbali kumpa contract deal kama member wa Tiptop connection na zawadi ya gari aliyompa hivi karibuni,ila Madee amekua na Dogo janja begabega katika kuhakikisha anatimiza malengo yake ya kimuziki.
Dogo Janja na Madee.
08.MAUA SAMMER & MWANA FA.
Mara kadhaa Maua Sammer,anaetamba na hit song yake “Mahaba niue”amekiri hadharani kuwa rapper Mwana FA ndie aliegundua uwezo wake na kumfungulia njia katika harakati zake za kimuziki na kwa kuthibitisha hilo,hata nyimbo ya kwanza ya mrembo huyu kuingia mainstream “So crazy”alimshirikisha Mwana FA.
Maua Sammer.
07.NYANDU TOZI & DUDUBAYA.
Rapper huyu kisiki kutoka kundi la B.O.B lenye maskani yake kinondoni,miaka ya nyuma alikua na ukaribu na Dudubaya,waliambatana kwenye shows kibao hata Dudubaya kwenye interview kadhaa alienda mbali zaidi na kumtaja Nyandu tozi,enzi hizo Dogo hamidu kama mwanae,japo kwa sasa Nyandu tozi amejitengenezea fun base yake yeye kama yeye,ila ukaribu wake na Dudubaya ulifanya watu wengi kumjua na kumfatilia.
Nyandu Tozi.
06.HARMONISER & DIAMOND.
Harmonizer anaetamba na hit songs kama “Aiyola”na “Bado”aliyomshirikisha Diamond,ni wazi hatasahau jina la Diamond Platnumz kwenye maisha yake,kwani licha ya kupata contact record deal ya WCB,label inayomilikiwa na Diamond,amekua akipata mashavu ya kwenda kwenye shows kubwa na Diamond,hata kwenye interviws kadhaa amekua akisindikizwa na Diamond Platnumz,kwa kudhihirisha hilo,Harmonizer ameamua kujichora tatoo ya jina Diamond kwenye kiganja chake cha mkono.
Harmonizer na Diamond.
05.NICK WA PILI & JOH MAKINI.
Rapper Nick wa pili,mmoja wa member wa kundi la Weusi,na miongoni mwa wanamuziki wasomi nchini,ni wazi wengi wetu tulimjua na kuanza kumfatilia pale aliposhirikishwa na kaka yake Joh makini kwenye hit song inayofahamika kama “Niaje ni vipi”,ukisikiliza verce ya Nick wa pili katika wimbo huo utagundua uwezo alionao katika uandishi ila ukweli unabaki palepale kuwa platform ya kaka yake kwa wakati huo ilitosha kumrahisishia njia kutoka kimuziki.
Nick wa Pili na Joh Makini.
04.RAYMOND & DIAMOND.
Raymond a.k.a Ray vanny kama anavyojiita kwa sasa,mbali ya kuwa mtunzi mahiri na kuwa member wa kundi la Tiptop chini ya manager Babu Tale ambae pia ni manager wa Diamond,amekua akipata support ya kutosha kutoka kwa Diamond,na kwa kuthibitisha hilo hata alipoachia track yake mpya inayoitwa “Kwetu”aliambatana na Babu Tale na Diamond kwenye vituo vya redio wakiutambulisha.
Diamond,Raymond na Babu Tale.
03.OMMY DIMPOZ & T.I.D (TOP BAND).
Hakuna asiejua uwezo wa Ommy Dimpoz awapo jukwaani,ila mwimbaji huyu ambae kwa sasa anatamba na hit song yake ya “Achia body” huku akimiliki music label yake ya PKP (Pozi kwa Pozi Ent.),kabla ya kuanza kuachia project zake mwenyewe,alikua chini ya Top Band inayomilikiwa na T.I.D,ni wazi kuwa Dimpoz ana vocal kali,ila pia kuwa kwenye band ya legend kama T.I.D ilikua platform tosha iliyompa connection na uzoefu katika muziki.
Ommy Dimpoz.
02.ABDUL KIBA & ALLY KIBA.
Abdul Kiba ambae ni ndugu wa damu wa Ally Kiba,alichukua headline kwenye music industry ya bongo pale alipoachia hit song inayofahamika kama “Kibela”aliyomshirikisha kaka yake,kama ilivyo kwa Nick wa pili na Joh Makini,ni wazi kuwa uwezo na umaarufu wa Ally Kiba,ulitosha kumfungulia njia Abdul Kiba katika harakati zake za muziki.
Ally Kiba na Abdul Kiba.
No comments:
Post a Comment