The Gunners wamefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali yamichuano ya FA Cup baada ya kuitupa nje Hull City kwa magoli 4-0 kwenye mchezo uliochezwa Jumanne usiku, shukurani ziende kwao Olivier Giroud pamoja na Theo Walcott ambao kila mmoja alitupia bao mbili nyavuni kwenye mchezo huo.
Story kubwa kwenye mechi hiyo ni ujumbe uliobebwa na mashabiki wa Arsenal wakimtaka kocha wao Arsene Wenger aachie ngazi kwenye timu yao.
November 2014, mashabiki wa Arsenal walibeba headlines baada ya kunyanyua mabango kwenye mchezo wao wa ugenini dhidi ya West Brom moja ya mabango hayo liliandikwa “Arsene, Thanks for the memories but it’s time to say goodbye”
Bango kama hilo lilonekana tena kwenye mchezo dhidi ya Hull licha timu hiyo kupata matokeo ya ushindi wa bao 4-0 wakiwa ugenini lakini mashabiki wameonesha kutoendelea kumuhitaji na hawana tena imani na Wenger kwenye kikosi cha Arsenal.
Ushindi wa Arsenal unaendelea kuwaweka katika nafasi nzuri katika michuano ya FA Cup na endapo watachukua kombe hilo msimu huu itakuwa ni mara ya tatu mfululizo.
Mchezo wa Premier League kati ya Arsenal dhidi ya West Brom uliopangwa kuchezwa Jumamosi umeahirishwa na kusogezwa mbele na badala yake siku ya Jumapili Arsenal itacheza mchezo wa robo fainali ya FA Cup dhidi ya Watford.
Rekodi zilizowekwa kwenye mchezo wa FA Cup kati ya Hull City dhidi ya Arsenal:
- Arsenal walipata goli kutokana na shuti lao la kwanza on target kwenye mchezo huo.
- Arsenal haijapoteza mchezo wowote wa FA Cup ikiwa ugenini dhidi ya timu za chini kwenye ligi, inarekodi ya kushinda michezo 12 na kutoka sare mara 4
- Arsenal wamechinda michezo yao yote sita iliyopita waliyocheza ugenini dhidi ya Hull kwenye mashindano yote wakifunga angalau magoli mawili kwenye kila mchezo.
No comments:
Post a Comment