Zaidi ya wapiganaji
150 wa Al-Shabab wameuawa kufuatia shambulizi la ndege isiyokuwa na
rubani ya Marekani katika maficho yao nchini Somalia.
Taarifa kutoka makao makuu ya usalama ya Pentagon inasema.Taarifa hiyo inasema kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa dhidi ya kambi moja ya Al Shabab takriban kilomita 195 Kaskazini mwa Mogadishu.
"Tulitekeleza shambulizi lililofaulu dhidi ya wanamgambo hao wa kiislamu wa Al Shaabab.'' alisema kapteni Jeff Davis.
Kundi hilo lilikuwa linajiandaa, kutekeleza mashambulizi ambayo yangetishia usalama wa majeshi ya Marekani na yale ya umoja wa Afrika.
Majeshi ya Afrika yaliwaondoa wapiganaji hao kutoka mijini mwaka wa 2011 hata hivyo kundi hilo limeendelea kuyashambulia kila kukicha kwa nia ya kuchukua madaraka.
No comments:
Post a Comment